Nyahunyo:Askari wa AP amemwajiri msichana wa miaka 14 kama kijakazi

Muhtasari
  • Wakikukosea au wakikosea jamii, huwa wanaletwa kwenye kitengo cha nyahunyo ili wapokee adabu na tabia zao kurekebishwa
  • Mwanamume mmoja alisimulia na kutaka askari wa AP apewe nyahunyo baada ya kumwajiri mtoto wa shule
Mbusi,Lion na DJ Gregg254
Image: Studio

Wakikukosea au wakikosea jamii, huwa wanaletwa kwenye kitengo cha nyahunyo ili wapokee adabu na tabia zao kurekebishwa.

Mwanamume mmoja alisimulia na kutaka askari wa AP apewe nyahunyo baada ya kumwajiri mtoto wa shule.

Kulingana na mwanamume huyo, askari huyo amekuwa akimlipa mtoto huyo elfu moja kwa mwezi.

"Nataka askari wa AP ambaye ni jirani yanu, apewe nyahunyo kwani amekosea jamii baada ya kumwajiri msichana wa miaka 14 kama kija kazi wake

Siku moja  nilimpata msichana huyo akilia, na kuniambia kwamba askari huyo amekataa kumrudisha nyumbani kwao na amekuwa akimlipa elfi moja kwa mwezi

Ni jambo amblo tunataka kulipeleka kwa chifu na kwa mzee wa nyjmba kumi kwa maana hajafanya vizuri, lakini kwanza nataka apewe nyahunyo kwa makosa hayo," Alieleza Jamaa huyo.