Mke wangu alisema kwamba nimepagawa,'Jamaa ataka mkewe apewe nyahunyo

Muhtasari
  • Jamaa ataka mkewe apewe nyahunyo
(Kushoto)Mbusi,(kati)DJ Nyce,(kulia) Mbusi
Image: Studio

Siku ya JUmatano jamaa alitaka mkewe apewe nyahunyo kwa madai kwamba ameshindwa kuweka siri za nyumbani kwake.

Kulingana na jamaa huyo mkewe amekuwa akitoa siri za nyumbani kwa majirani na kusema kwamba amepagawa kwani amekuwa akitoa usiku wa manane na kuenda kazini.

"Nataka mke wangu apewe nyahunyo kwani ameshindwa kuweka siri za nyumbani, nafanya kazi ya dereva, ambapo huwa natoa usiku wa manane na kuenda kazini

Nilikuwa nimelala siku moja mchana nikaskia akiwaambia wanawake wake wenzake kwamba mimi ni mepagawa kwa maana nimekuwa nikienda kazi usiku, na narudi nyumbani usiku, kwa hivyo nahitaji maombi," Alieleza.

Je mwanamke huyo alistahili nyahunyo au la?