Rafiki yangu alitoroka na mke wangu-Jamaa ataka rafiki yake apewe nyahunyo kwa kulamba asali ya mkewe

Muhtasari
  • Wakikukosea na kukosea jamii, huwa tunawapa nyahunyo na kurekebisha makosa yao katika kitengo cha Nyahunyo
(Kushoto)Mbusi,(kati) DJ Nyce, (kulia) Mbusi
Image: studio

Wakikukosea na kukosea jamii, huwa tunawapa nyahunyo na kurekebisha makosa yao katika kitengo cha Nyahunyo.

Siku ya Jumanne jamaa alitaka rafiki yake apewe yahunyo baada ya ya kulamaba asali ya mkewe na kutoroka naye.

Kulingana na jamaa huyo, mwanamume uyo anafahamika sana, na licha ya kuwa na familia na watoto alitoroka na mkewe baada ya yake kuumia.

"Nataka rafiki yangu apewe nyahunyo kwa kutoroka na mke wangu, alikuwa ananiletea matunda baada ya kupata ajali na kuumia kwenye magoti

Sikuwa nafahamu kuwa wana uhusiano na mke wangu, marafiki zangu ndio waliniambia,kisha nikawapata kwenye chumba pamoja wakifanya tendo la ndoa

Ni mwanamume ambaye ana familia yake na mtoto, niliuwa nimebarikiwa na mtoto mmoja na mke wangu," Alieleza.

Je jamaa huyo alistahili nyahunyo, au wote wawili walistahili kupewa nyahunyo kwa kutoroka pamoja?