Jamaa aliyejitambulisha kama Kingsley Ogwaku ,26, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Prisicah Adema ,24, ambaye alikosana naye mwishoni mwa mwaka uliopita.
Kingsley alisema mkewe alitoroka ndoa yao ya miaka minne mwezi Disemba baada ya kumpata akizungumza na jamaa mwingine kwenye simu.
"Ilikuwa mwezi Disemba mwaka jana. Niilikuwa nimenunulia simu. Wakati nilitoka kazi saa tatu usiku nilipata anachat na jamaa kutoka FB. Nilipomuuliza huyo ni nani, alisema hamjui na hata amemblock," Kingsley alisimulia.
Aliongeza, "Baadaye kidogo nikapata anapigiwa simu. Nikataka kushika alafu roho ikanikataza. Huyo jamaa akakataa. Ile harakati ya kumnyang'anya simu ikawa ni vita. Baadaye akasema huyo ni jamaa ambaye alikuwa amuunganishe na kazi. Keshoye nikitoka kazi nikapata ameenda."
Alidai kwamba baada ya kufanya uchunguzi alipata ushahidi wa kutiliwa shaka kuhusu uhusiano wa mkewe na jamaa huyo.
"Mtu mpaka anamuuliza uko aje? umekula nini? mpaka anamtumia namba ya simu? Nilipofanya utafiti wangu nilipata amepigwa picha na huyo jamaa. Mara ya mwisho nilimuona Kibra. Nikimpigia simu naona ameniblock," alisema.
Priscah alipopigiwa simu, Kingsley alichukua nafasi hiyo kumhakikishia kuhusu upendo wake kwake na kumuomba arudi.
"Priscah mimi nakupenda na tumetoka mbali. Nakupigia simu na umeniblock. Nimeamua nikusamehe kwa makosa ulifanya," alisema
Priscah alikanusha kumfahamu jamaa ambaye namba yake ilipatikana kwenye simu yake na akamshtumu mpenziwe kwa ulevi.
"Ana tabia mbaya sana. Analewa anarudi kwa nyumba saa tisa usiku. Ata hajui umeshinda aje. Ukimuuliza anasema alianza kulewa akiwa mdogo hawezi kuacha. Akipata pesa huoni anapeleka wapi. Nilikaa nikatoka, nikasema njaa itaniua nitoke. Anapata pesa ndio lakini akipata huoni inaenda wapi," Priscah alisema.
Kingsley alimwambia, "Mimi nilitaka nikusamehe. Mimi nakupenda kama asali, rudi nyumbani tuendelee."
Priscah hata hivyo alisema, "Nilikuona unatembea na msichana, bado hujamuoa?.. Mimi ata nilikuwa nimemsahau kwa sababu ya mambo amenifanyia. Na miaka yangu siwezi kubali mlevi na kuwekwa njaa kwa nyumba."
Kingsley alipuuzilia mbali madai ya kutonunua chakula kwa nyumba na akamshtumu mpenziwe kwa kutumia mafuta lita 10 kwa mwezi.
"Nilikuwa namnunulia mafuta lita 10 anamaliza na mwezi moja!" Kingsley alisema.
Priscah hata hivyo alibainisha kwamba mumewe alikuwa ananunua mafuta lita moja tu.
Baada ya wawili hao kutoelewana, Kingsley alisema, "Nilikuchukua msichana nitembee kwake asiletee mguu kwangu."
Priscah kwa upande wake alisema, "Nakutakia maisha mema lakini ubadilike. Hakuna msichana ambaye anaweza kuvumilia na hiyo tabia."