PATANISHO:Mke wangu aliniacha baada ya yangu kutoka nje ya ndoa

Muhtasari

•Mke wangu alipojifungua hakuwa na hamu ya ndoa, hakuwa ananipikia kiamsha kinywa nikienda kazini

•Frank ana hasira nyingi alini mwangia maji baridi,Amekuwa akileta wanawake kwa nyumba

•Nilikuwa nazungumza na wanawake wengine kimaksudi ili mke wangu aweze kunitamani tena

 

 

Gidi na Ghost

Leo hii katika kitengo cha patanisho bwana Frank alituma ujumbe ii apatanishwe na mkewe mama Jayden ambaye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka miwili.

"Tulikosana na mke wangu mwezi jana baada ya yangu kutoka nje ya ndoa, baada ya mke wangu kujifungua kulikuwa na shida nilimpa miezi sita ili aweze kupona

baada ya kupona mke wangu hakuwa na hamu ya tendo ya ndoa, jambo hilo ndilo lilinikusudia na kunichangia niende nje ya ndoa lakini nilikuwa nafanya kimaksudi ili mke wangu aweze kuona kuwa ananitesa

 

Pia alibadilika kabisa hata hakuwa ananipikia kiamsha kinywa, na mshawishi lakini hakuweza kunisikia

Naomba turudiane kwa maana ninaumia sana na mambo hutendeka." Alieleza Frank.

Lakini kwa kawaida lazima kila mmoja ajitetee na kuficha siri fulani, mama Jayden naye alikuwa na haya ya kusema.

"Frank ana hasira nyingi sana anaweza amka siku moja asubuhi na kisha ananipiga, wazazi wangu walimwambia kuwa aje kwetu wamuone

Wakati kafyu ilikuwa ya saa tatu alikuwa ananiletea pesa saa tatu na kuniambia nitoka nikanunue chakula

Kuna wakati nilienda kumripoti kwa polisi na kuwaambia hamna kitu ambacho amenifanyia nilitembea mguu kutoka umoja hadi Karen

itu ambacho kilinifanya nitoke kuna wakati alinimwagia maji baridi na hata kuleta wanawake kwa nyumba, kama anataka turudiane aje nyumbani kwetu Sultan kwa wazazi na abadilishe tabia zake."