PATANISHO:Mpenzi wangu aliniacha baada ya kupata kondomu chini ya kitanda

Muhtasari
  • Nilikosana na mpenzi wangu baada ya yake kupata kondomu chini ya kitanda
  • Mimi si mtoto wake wa kuchezea kila wakati Christine alisema 
Gidi na Ghost

Bwana Brian,26, alituma ujumbe katika studio zetu ili apatanishwe na mkewe Christine 25 wake ambaye walikosana kwanza kwa kutomlipia mahari na jambo la pili  baada ya kupata kondomu zilizitumiwa chini ya kitanda yao.

"Nilikosana na mke wangu baada ya yake kuchokora nyumba na kupata kondomu ambazo zimetumiwa chini ya kitanda tulikosana wiki mbili zilizopita

nataka nimuombe msamaha kwa maana sijawahi paa msichana kama yeye maishani mwangu." Alieleza Brian.

Haya basi lazima kila mtu afiche ukweli kwa upande wake, haya basi tulipofanya juhudi zetu za kumpigia mkewe au mpenzi wake alikuwa na haya ya kusema,

"Mimi naishi Nairobi na yeye anaishi Limuru kila niendapo kumtembelea napata vitu vya wanawake kuna wakati nilipata kondomu chini ya kitanda juzi sasa nilipata shati la mwanamke nilipomuuliza aliniambia kuwa ni za ndugu yake

Kila kitu nikipata anasema ni za ndugu yake, mimi nimechoka kabisa na mambo yake sitaki wacha akae hivyo mimi si mtoto wake wa kuchezea kila wakati

Kuna wakati nilimpigia simu  ikapokelewa na mwanamke akaniambia mwenye simu hayuko nilipopiga simu mara ya tatu alipokea simu." Alisema Christine.

Bwana huyo alisema kuwa hayuko tayari kuachana na mpenzi wake baada ya yake kukata kauli hataki kurudiana naye

Kwa mengi zaidi tembelea mitandao ya youtube kwa uhondo zaidi.