PATANISHO: Nilikosana na mama mkwe baada ya kumtumia mke wangu nauli na kwenda kwao na kuniachia watoto

Muhtasari
  • Nilikosana na mama mkwe baada ya kumtumia mke wangu nauli
  • Alimtoa mtoto wangu akiwa darasa la sita, na hata hajui kwa mke wake na hanijui
Gidi na ghost
Gidi na ghost Gidi na ghost
Image: radiojambo

Bwana Ochieng alituma ujumbe katika studio zetu apatanishwe na mama mkwe ambaye walikosana naye miezi mbili iliyopita.

"Nimeoana na mke wangu kwa miaka kumi sasa nilikosana na mama mkwe baada ya kumtumia mke wangu nauli na kurudi kwao ilhali alikuwa na mtoto wa miezi kumi na moja

Mke wangu aliniachia watoto wote wanne na kurudi kwao, nilimtumia nauli tena baada ya muda na akarudi tena sasa niko naye kwangu

Nilimtumia jumbe na kumwambia amtafutie mke wangu mume mwingine, mke wangu aliporudi aliniambia kuwa mama mkwe amekasirika sana." Alieleza Ochieng.

Baada ya kufanya juhudi zetu na kumpigia mama mkwe naye kwa upande wake alikuwa na haya ya kusoma.

"Alkuwa anamtesa mtoto wangu, alimtumia nauli na kisha akatoroka bila ya kuniambia, mimi nimewaombea baraka zake Mungu

Ni miaka kumi lakini bwana Ochieng hanijui wala hajui nyumbani kwa mke wake, mimi nimemsamehe lakini afanye juhudi za kuleta mahari, kwa maana si vyema kuoa binti ya mtu kwa miaka yote bila ya kujua kwao

Alimtoa mtoto wangu akiwa darasa la sita."