Patanisho:Niliachana na mume wangu baada kugundua anatumiwa jumbe na wanawake

Muhtasari
  • Mume wangu amekuwa akiniambia kuwa nafuatilia maisha yake sana napaswa kuachana nayo
  • Amekuwa akija nyumbani kama amechelewa wakati mwingine napata jumbe za wanawake kwa simu yake
patanisho
patanisho

Bi Jackline alituma ujumbe ili apatanishwe na mume wake Felix wiki mbili zilizopita baada ya mzozo wa familia.

"Nilikosana na mume wangu baada ya yake kuzoea kuja nyumbani akiwa amecelewa, wiki mbili zilizopita mume wangu alinipigia simu na kuniambia anachelewa nilimjibu na hasira na kumwambia nishaa mzoea

Pia alikuwa ananiambia kuwa yeye ni mwanamume ana ruhusa ya kurejea nyumbani saa zenye anataka, alikuwa anatumiwa jumbe na wanawake wengine

 

Tulipokosana alikuja nyumbani na kubeba nguo zake na kupeleka kwa ndugu yake." Alieleza Bi Jackline.

Baada ya kufanya juhudi za kumpigia Felix alisema ya kwamba amechoka na mambo hayo.

Kama mwanajambo utampa Jackline ushauri upi kuhusu kesi yake?