PATANISHO: Mke wangu aliniacha baada ya mimi kuanza kurudi nyumbani nikiwa nimechelewa

Muhtasari
  • Mume wangu alinitumia namba ya mwanamke mwingine na kuniambia kuwa anamsumbua nimpigie simu
patanisho
patanisho

Leo katika kitengo cha radiojambo bwana Philip alituma ujumbe apatanishwe mkewe ambaye walikosana naye wiki jana.

"Nilikosana na mke wangu wiki mbili zilizopita baada ya yangu kuanza kurudi nyumbani nimechelewa 

Sijui ni kama aligadhabishwa na hiyo tabia na kutoka kwa nyumba, nikimpigia simu ananiambia atarudi nyumbani." Alieleza bwana Philip.

 

Katika kila upande lazima kila mmoja ataficha makosa yake naye mkewe alikuwa na haya ya kusema;

"MUme wangu alinitumia namba ya simu ya msichana mwingine na kuniambia kwamba huyo msichana anamsumbua

Kwanini hakunipa namba nikiwa naye ananiumia nikiwa nimetoka, pia huyo msichana aliniambia kuwa Philip alimtumia nauli aende kwake lakini alipokataa kuenda akaanza kumtusi

Sawa nitarudi kabla ya Desemba."