Patanisho: Nilikosana na shemeji yangu kwa ajili ya kuchukua watoto wangu

Muhtasari
  • Shemeji yangu aliniambia kuwa natesa watoto wangu kwa maana mimi si baba yao mzazi
Gidi na Ghost

Leo katika kitengo cha patanisho bwana Titus alituma ujumbe ili apatanishwe na shemeji yake ambaye walikosana bada ya yake kuchukua watoto wangu bila yangu kujua wala kufahamu.

"Nilikosana na shemeji yangu baada ya yake kuchukua watoto wangu na kuenda kuishi nao, nilipomuuliza aliniambia kuwa nilikuwa natesa watoto wangu

Watoto hao wawili walikuja na mke wangu, mimi si baba yao mzazi."Alieleza Titus.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumtafuta shemeji yake alikuwa na haya ya kusema.

"Ambia huyo mwanamume anitafute kwangu kwa maana anapajua, kuna mambo mengi ya kuzungumzia na bado anaishi na dada yangu."

Swali kuu ni je amekuwa akiwatesa watoto hao au la kwa maana bwana huyo amesema kwamba alikuwa tu anamuhadhibu mwanawe wa kwanza kwa maana alikuwa mtundu.