PATANISHO: Nilikosana na ndugu yangu baada ya yeye kudai kuwa nilimyang'anya mpenzi wake

Muhtasari
  • Nilikosana na ndugu yangu baada yake kudai kuwa nilimyang'anya mpenzi wake
  • Kwa sasa mwanamke huyo ni mke wangu
Gidi na Ghost

Bwana Joshua alituma ujumbe apatanishwe na ndugu yake Maxwell ambaye walikosana mwaka jana baada ya kuchukua mwanamke ambaye aliyedai ni wake.

"Nilikosana na ndugu yangu mkubwa mwaka jana baada ya yake kudai kuwa nilinyakua mwanamke wake

Nilipomuuliza mwanamke huyo aliniambia kuwa hakuwa amempenda bali ni mimi alikuwa ananipenda nilimpigia simu akaniambia nisiwahi enda nyumbani

Mwanamke huyo sasa ni bibi yangu." Alieleza Joshua.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia Maxwell alisema kwamba jambo hilo lilimuumiza sana licha ya yake kumpenda mwanamke huyo.

"Jambo hilo liliniumiza sana mpaka hadi leo sijawahi penda mwanamke mwingine, alininyang'anya mpenzi wangu

Nilikuwa nimeeka kama sure bet lakini ikashindikana, kama anataka tuzungumze aje pekeyake ili tuzungumze kwa maana akija na huyo mwanamke atanipa kumbukumbu

Alinifanya madharu sana." Alisema Maxwell.