Patanisho:Mke wangu alinidanganya baba yake ameaga dunia,ameavya mimba yangu

Muhtasari
  • Mwanamume aeleza jinsi mkewe aliavya mimba yake, huku akimdanganya kuwa baba yake ameaga dunia
Gidi na Ghost

Katika kitengo cha patanisho bwana Godfrey alituma ujumbe apatanishwe na mkewe ambaye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka 4.

Wawili hao walikosana mwaka jana baada ya mkewe kuenda kwao bila idhini ya mumewe.

"NImekuwa kwa ndoa na mke wangu kwa miaka 4 tulikosana mwaka jana, baada ya kuenda kwao bila idhini yangu

 

Nilipompigia simu arudi nyumbani alinidanganya kwamba baba yake ameaga dunia ilhali ilikuwa uongo, nilipofuatilia nilipata kuwa aliavya mimba yangu

Pia nasikia kwamba ameenda nairobi kufanya kazi," Alieleza bwana huyo.

JUhudi za kumpigia mkewe ziliambulia patupu kwa maana mkewe hakushika simu, kwa maana ilikuwa mteja.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo youtube.