Patanisho:Nilimtusi mama yangu nikiwa mlevi sasa niko ndani kwa ajili ya hayo

Muhtasari
  • Katika kitengo cha patanisho, bwana Wickman alituma ujumbe ili apatanishwe na mama yake baada ya kuenda korokoroni baada ya kumtusi mama yake

Katika kitengo cha patanisho, bwana Wickman alituma ujumbe ili apatanishwe na mama yake baada ya kuenda korokoroni baada ya kumtusi mama yake.

Alifanya kitendo hicho mwaka huu Aprili,9.

"Nilimtusi mama yangu baada yangu ya kurudi nyumbani nikiwa mlevi mwaka huu Aprili, hakupendezwa na tabia zangu aliwaita polisi na nikatiwa korokoroni nilipelekwa mahakamani na nikahukumiwa

Nataka kuomba mama yangu msamaha kwa maana nilimkosea mama yangu sana," Alieleza bwana Wickman.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia mama yake, alisema kwamba aliamua sheria ichukue mkondo wake na kuwa amemzoea sana.

Pia alifichua kwamba Wickman alimtusi sana huku akimuita malaya na mchawi licha yake ya kuwa amemzaa.

"Wacha afanye vile anataka kwa maana nilimuonya mara nyingi sana kwa ajili ya tabia zake, nimechoka nilifanya majukumu yote kama mama na baba

Alinitusi kuwa mimi ni malaya na mchawi, sijawahi mchukia mtoto huyo, mimi nimeamua sina mtoto hata ndugu zake wamesema hawana uhusiano naye," Alieleza mama huyo.

Mama alisisitiza kwamba hatomsamehe mtoto huyo kwa maana alimuonyesha njia ya maisha lakini hakusikia.

Kwa mengi zaidi tembelea Radio jambo Youtube.