Patanisho:Nilitumia pesa za karo kumpeleka mpenzi wangu 'out'

Muhtasari
  • KIjana ajuta kumpeleka mpenzi wake 'out' na pesa ya karo
  • Kulingana na kijana huyo baada ya kumpeleka mpenzi wake 'Out' walishikwa na polisi ambapo baba yake alitoa pesa zaidi ili waachiliwe
Ghost na Gidi
Image: Studio

Leo katika kitengo cha patanisho, kijana Ian alituma ujumbe ili apatanishwe na baba yake baada ya kutumia pesa za karo alizokuwa amepewa.

Kulingana na kijana huyo baada ya kumpeleka mpenzi wake 'Out' walishikwa na polisi ambapo baba yake alitoa pesa zaidi ili waachiliwe.

"Nataka kupatanishwa na baba yangu, tulikosana baada yangu kutmia pesa ya karo kumpeleka penzi wangu 'outing'

Niliamka usiku wa manane na nikaenda kukomboa pikipiki na tukaenda out, tulipokuwa tukinywa soda tulishikwa na polisi na tukaenda kucharazwa kwa maana walitambua kwamba msichana niliyekuwa naye alikuwa wa shule

Baba yangu alikuja akatoa shilingi elfu nane ili tuahiliwe, kesho yake msichana huyo alikuja kwetu na tukalala kwetu kutoka siku hiyo tukakosana na baba yangu na nikataoroka nyumbani," Alielea Ian.

Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia baba yake simu alikuwa na haya ya kusema;

"Nilisikitika sana na matendo yake, kiburi yake ndio ilifanya maendo yake, nilitaka arudi shule lakini akatoroka,nishaamsamehe kwa hivyo arudi nyumbani aende shuleni,"Mudami Alisema.