Patanisho:Mume wangu anasema namchunga sana ilhali natekeleza majukumu ya mke

Muhtasari
  • Mume wangu anasema namchunga sana ilhali natekeleza majukumu ya mke

Bi Cynthia alituma ujumbe ili apatanishwe na mume wake Hassan ambaye hawajakuwa wakiskiana naye kwa muda.

Kulingana na mwanamke huyo, mume wake amekuwa akilalamika kwamba anamchunga bali anatekeleza majukumu ya kuwa mke wake.

"Naomba mnipatanishe na mume wangu. Mimi ni mke wake wa pili. Hatuelewani kwa nyumba kwa sababu analalamika eti ninamchunga sana na simchungi... Juzi aliniambia yuko steji na kutoka huko mpaka kwa nyumba ni karibu dakika sita ila ilimchukua saa moja na dakika 30 kufika kwa nyumba..." Alielleza Cynthia.

Baada ya kufanya juhudi za kumpigia mumewe alikuwa na haya ya kusema.

"Wakati huo sikuwa kwenye kituo cha basi,na sina shida naye na pia nampenda,"Hassan alisema.