Patanisho:Mke wangu aliniacha baada ya mimi kuenda kutazama mpira

Muhtasari
  • Mke wangu aliniacha baada ya mimi kuenda kutazama mpira
Gidi na Ghost
Image: studio

Katika kitengo cha patanisho bwana Abraham alituma ujumbe apatanishwe na mkewe Achieng ambaye walikosana mapema mwaka huu.

Kisa cha kukosana ni kipi?

Kulingana na Abraham mkewe alimuacha baada yake kuenda kutazama mpira na kurudi nyumbani saa sita ya usiku.

"Nilienda kutazama mpira saa mbili usiku, nilirudi saa sita ya usiku nilipofika nilimuamsha mke wangu nikamsalimia

Alikasirika na kuniambia kwamba wakati nimemalizana na wanawake wangu ndio narudi kwake, kesho yake aliamka na kuniachia watoto, kitinda mimba ana mwaka mmoja na miezi tisa

Nilimpigia simu na akarudi na kumchukua kitinda mimba na kuniacha na kifungua mimba wa miaka sita, ananishuku nina wanawake wengine kwa sababu mwaka wa 2018, nilipata mtoto nje ya ndoa nilimuomba msamaha na akanisamehe," Alieleza.

Baada ya kufanya juhudi za kumpigia mkewe alikuwa na haya ya kusema;

"Siyuko tayari kuzungumza,aliporudi nyumbani nilimuuliza mbona anatazama mpira mpka usiku,akaanza kugombana,nikaona hamna haja ya kukaa hapo nilimwambia akimaliza shughuli anitafute,"Aliongea Achieng.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.