Patanisho:'Nimemtumia zaidi ya milioni akuje na hakuji!' Jamaa asimulia vile amekuwa akitumiwa vibaya na 'Ex'

Erick Wasonga ambaye ni mhudumu wa bodaboda alidai kuwa mkewe kwa jina Moraa alimuacha baada ya kifo cha mtoto wao.

Muhtasari

•Bw Erick alidai kuwa tangu Moraa aondoke pale nyumbani amekuwa akimpigia simu akimsihi kurudi nyumbani  ila juhudi zake hazijawahi kufua dafu.

•Jamaa huyo alidai kuwa licha ya kutengana kwao mkewe amekuwa akimpigia simu kumuomba pesa akiahidi kurejea nyumbani pale baada ya siku chache ila kila anapojaribu kumpigia simu tena kuumuliza kuhusu agano lao hashiki.

Gidi na Ghost

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho siku ya Ijumaa mwanaume mmoja aliomba kupatanishwa na mkewe waliyetengana zaidi ya miaka tatu iliyopita.

Erick Wasonga ambaye ni mhudumu wa bodaboda alidai kuwa mkewe kwa jina Moraa alimuacha baada ya kifo cha mtoto wao. Alisema kuwa anampenda sana mwanamke huyo.

Bw Erick alidai kuwa tangu Moraa aondoke pale nyumbani amekuwa akimpigia simu akimsihi kurudi nyumbani  ila juhudi zake hazijawahi kufua dafu.

"Alienda kwao.. nimekuwa nikimfuatilia ila amekuwa tu na ukora mingi. Anasema ningoje kidogo nimpatie miaka miwili inaisha, tena kidogo  kidogo nimpatie mwaka mmoja tena ikaisha... nataka niskie kama anaweza rudi leo ama kesho. Huwa nimempenda." Erick aliambia Gidi.

Jamaa huyo alidai kuwa licha ya kutengana kwao mkewe amekuwa akimpigia simu kumuomba pesa akiahidi kurejea nyumbani pale baada ya siku chache ila kila anapojaribu kumpigia simu tena kuumuliza kuhusu agano lao hashiki.

"Gidi huyo mtu hasemi ukweli. Akiwa na shida kila siku ananipigia simu ananiambia Erick nitumie kama elfu mbili hivi nikuje Jumatatu. Ikifika Jumatatu hashiki simu," Erick alidai.

Alisema kuwa huwa anamtumia mwanamke huyo pesa akiwa na imani kuwa angerudi wakae pamoja.

Hata hiyo, Moraa ambaye aliskika kutoridhishwa na hatua ya Erick kujaribu kupatanasishwa tena na yeye alidai kuwa alikuwa ameshasonga mbele na maisha na kuolewa na mume mwingine.

"Mimi nilishasonga mbele kitambo" Moraa aliambia Gidi.

Erick ambaye alisikika kukasirishwa na habari hizo aliapa kuwa atatafuta mke mwingine aoe.

Jamaa huyo alieleza masikitiko yake kuona kuwa kulingana na hesabu yake jumla ya pesa zote alizokuwa ametumia Moraa kutoka mwaka wa 2016 akiahidi kuja ilikuwa imekuwa imefikia shilingi milioni moja.

"Ukipiga hesabu hiyo elfu mbili nimetuma kutoka 2016 saa hii imefika hata milioni moja. Unajua huwa natuma mara mingi kwa mwezi mmoja akiahidi kuja na hakuji!" Erick alisema kwa hasira.

Gidi alimshauri Erick kusita kutuma pesa kwa Moraa kwani ilionekana kama kwamba amekuwa akimtumia vibaya. Gidi pia aliwaomba wanawake kukoma kutumia wanaume vibaya na kula nauli wanapotumiwa na wenzao wanaume.