Patanisho:Mke wangu alininyima haki yangu,aliniambia tuishi kama majirani

Muhtasari
  • Mke wangu alininyima haki yangu,aliniambia tuishi kama majirani
  • Kulingana na Onyango walikosana baada yake kumpeleka mtoto wake kwa nyanya yake,hii ni baada ya mke wake kumgombesha mtoto huyo
Gidi na Ghost
Image: Studio

Katika kitengo cha Patanisho siku ya Ijumaa bwana Onyango alituma ujumbe apatanishwe na mke wake Akinyi ambaye walikosana naye baada ya kuwa kwa ndoa kwa mwaka mmoja.

Kulingana na Onyango walikosana baada yake kumpeleka mtoto wake kwa nyanya yake,hii ni baada ya mke wake kumgombesha mtoto huyo.

"Naomba mnipatanishe na mke wangu. Nilimuoa na watoto nami pia nilikuwa nimeachiwa wangu na mke wangu wa kwanza

Akagombeza mmoja kumuuliza, tukakorofishana akaanza kulala chumba kingine akisema tuishi kama majirani. Nikahamia kwingine kwa kuninyima tendo la ndoa

Pia naye alikuja na watoto 3," Alisema Onyango.

Baad ya kufanya juhudi zetu za kumfikia mkewe, alikuwa na haya ya kusema;

"Alipotoka nyumbani hakuniambia anaenda wapi, alibeba bidhaa za nyumbani unaniambia niende nyumbani na nikiwa Kericho hunitumii pesa, mwalimu akikupigia simu kwa ajili ya karo ya shule unasema kwamba ni 'wrong number'

Hajui mimi mkewe nakula nini wala watoto wanaenda aje shuleni, nimekuwa nikifanya vibarua ili kujikimu," Akinyi alieleza.

Kwa uhondo zaidi tembelea Radiojambo Youtube.