Patanisho:Mungu ndiye huleta mwanamume na mwanamke pamoja,jamaa asema baada ya kugundua mkewe ameolewa tena

Muhtasari
  • Katika kitengo cha patanisho bwana Joseph alituma ujumbe apatanishwe na mkewe ambaye, walikuwa katika ndoa kwa muda wa miaka 8
Ghost Mulee na Gidi
Image: Radiojambo Studio

Katika kitengo cha patanisho bwana Joseph alituma ujumbe apatanishwe na mkewe ambaye, walikuwa katika ndoa kwa muda wa miaka 8.

Kulingana na Joseph, mkewe alimuacha baada yake kuangusha biashara, na mkewe kufukiria na kusikia fununu anaharibu pesa na wanawake.

"Naomba nipatanishwe na mke wangu wa miaka 8, nilikosana naye baada ya biashara ambayo nilikuwa nimesiamamia kuanguka

Ilikuwa biashara ya samaki, na ni kweli biashara ilianguka lakini sikutumia pesa na wanawake,Mungu aliumba mwanake kwa ajili ya wanaume, na akaumba mwanamume kwa ajili ya wanawake, na ni yeye tu huwaleta hawa watu pamoja

Kama ameolewa ni sawa siwezi pinga," Joseph alisema baada ya kugundua mkewe ameolewa tena.

Baada ya kufanya juhudi za kumfikia mkewe alikuwa na haya ya kusema;

 

"Kama anajua vyema alifanya biashara ianguke, mbona asinitafute."

Mkewe alimpa mumewe simu na kisha akasema kwamba ameolewa na Joseph anapaswa kukoma kumsumbua mkewe.

"HUyu mwnamke ameolewa, ni mke wangu na mwambia Joseph kwamba awache kumsumbua mke wangu kwani tuna furaha katika ndoa yetu na tunatarajia kifungua mimba wetu."

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo youtube.