Patanisho:Jamaa amkasirikia mkewe kwa kuchukua simu yake na kumkosanisha na mpango wa kando

Muhtasari

•Irene alisema hata kama bado hajatengana na mumewe, alikuwa amechoka na maisha kwa kuwa hakujakuwa na hali ya kuelewana katika boma lao kwa kipindi cha miezi miwili.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi mwanadada aliyejitambulisha kama Irene (22)  akiomba kusaidiwa kurejesha mahusiano mazuri kati yake na mumewe Nicodemus (29). 

Irene alisema hata kama bado hajatengana na mumewe, alikuwa amechoka na maisha kwa kuwa hakujakuwa na hali ya kuelewana katika boma lao kwa kipindi cha miezi miwili.

Alieleza kwamba mumewe ambaye wamekuwa naye kwenye ndoa kwa kipindi cha mwaka mmoja alianza kubadilika wakati alipochukua simu yake na kusoma jumbe alizokuwa ametumiwa na wanadada wengine.

"Mume wangu amefika mahali amebadilika. Kwa nyumba hakuna mapenzi. Akitoka kazini anaingia kwa nyumba akiwa amenuna. Nikimuuliza shida ni nini anasema hakuna ila nikimwangalia naona ako na stress. Inafika mahali nashangaa pengine nilimkosea na hataki kuongea juu amenuna tu. Ilianza mwezi wa kumi na moja mwaka uliopita  wakati nilianza kupata jumbe kwa simu yake. Zilikuwa jumbe za mapenzi, kuna msichana  alikuwa anamtumia. Nilipomuuliza  alisema kwamba kabla hatujakutana na yeye alikuwa ameambia dadake amtafutie msichana. Aliniambia eti ameachana nao" Irene alisema.

Irene alisema baada ya kugundua mumewe alikuwa anatumiana jumbe za mapenzi na wanawake wengine alijaribu kumshinikiza  akome tabia ile.

Alifichua kwamba mvurugano zaidi uliibuka baada yake kuchukua simu ya mumewe  na kumtenganisha na mpango wake wa kando kupitia ujumbe.

"Hakuwahi kuwa hivo. Ile siku alileta shida  ni vile niliandikia msichana ujumbe kutumia namba yake. Nilijifanya mimi ni yeye nikamwambia sina ubaya na yeye na niko na bibi na mtoto. Nilimwandikia aache kutuma jumbe kwa sababu sitaki kukosana na bibi yangu. Alienda kazi alafu kurudi  akaja akiwa amenuna. Aliniuliza ni ujumbe gani nilitumia msichana wa wenyewe" Alisema.

Nicodemus alipopigiwa simu alisikika mwenye wasiwasi na alisita kunena sana na mkewe ili kusuluhisha mzozo wao.

Irene hata hivyo alisema mumewe alikuwa amemhakikishia kwamba aliacha mambo ya mpango wa kando.

Aliomba mumewe akubali hali ya kuelewana irejee kati yao huku akimhakikishia kuwa anampenda sana.