PATANISHO:Kama mke ni wewe heri nife bila mke-Mwanamume amkataa mkewe hata baada ya kuomba msamaha

Muhtasari
  • Kulingana na Mapenzi sababu kuu ya kukosana ni kwa ajili alihudhuria mazishi ya mama yake, licha ya mumewe kumkataza
Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha patanisho Bi Esther Mapenzi, alituma ujumbe ili apatanishwe na mumewe ambaye walikosana mwaka wa 2016.

Kulingana na Mapenzi sababu kuu ya kukosana ni kwa ajili alihudhuria mazishi ya mama yake, licha ya mumewe kumkataza.

"Ulikuwa mwaka wa 2016 ambapo nilikosana na mume wangu,niliavhana naye baada ya mama yangu kuaga dunia, lakini alinikataza kuenda katika mazishi hayo, kwa maana nilikuwa mjamzito

Niliposisitiza kuenda aliniuliza kama nikienda mama yangu atafufuka, nilienda na akaniambia niishi kwetu kwani niligeuka maagizo yake

Ninapomuuliza mambo ya kurudiana aliniabia kwamba nikipata mwanamume naweza kuolewa, ilhali nina watoto 4 wake," Bi Mapenzi Alisimulia.

Baada ya kufanya juhudi za kumfikia mumewe bwana Kyalo, aliweka wazi kwamba hataki kumrudia mkewe heri afe bila mke.

"Kama mke ni huyu haya basi wacha nife bila mke, ata makasisi hukaa bila wake nimekuwa nikilea watoto,nenda uolewe, mama Triza ni msichana mrembo lakini tabia hapana kila mwisho wa mwaka amekuwa akikusanya virago na kuenda kwao

Umelelewa vizuri na wazazi wazuri lakini tabia yako mbovu," Bwana Kyalo amesema huku akisema kwamba hataki kurudiana na mke wake.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.