"Niko na maisha yangu, nilishaolewa!" Mwanadada amvunja moyo jamaa aliyetangana naye miaka 6 iliyopita

Muhtasari

•Martin alidai ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika mwaka wa 2016 baada ya aliyekuwa mkewe kuavya ujauzito na kutusi mama yake.

•Esther alifichua kuwa kilichomshinikiza kugura ndoa ni kwa kuwa Martin alikosa uaminifu, alikuwa mlevi na mwenye vurugu.

•Esther alidhihirisha wazi kuwa hakuna uwezekano wake  kurudiana na Martin kwa kuwa tayari ameolewa na mwanaume  mwingine.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho jamaa aliyejitambulisha kama Martin ,30, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mkewe Esther ,26,  ambaye walitengana naye miaka sita iliyopita kufuatia mzozo wa kinyumbani.

Martin alidai ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika mwaka wa 2016 baada ya aliyekuwa mkewe kuavya ujauzito na kutusi mama yake.

Alikiri kuwa baada ya kutengana na Esther alijaribu ndoa na mwanamke mwingine ila haikufua dafu na ndiposa angependa mkewe arudi.

"Tulikuwa tumezungumzaia kupanga uzazi lakini akakataa. Baadae alipata ujauzito, mimi sikuwa tayari kupata mtoto mwingine. Alienda akaiavya... Baada ya kukosana alienda akachukua watoto kwa nguvu kutoka kwa wazazi wangu nami nikakataa kuwasaidia. Tumekuwa tukiongea kijuujuu tu lakini hatuelewani. Ako tu sigle, huwa ananiambia" Martin alisema.

Esther alipopigiwa simu alifichua kuwa kilichomshinikiza kugura ndoa ni kwa kuwa Martin alikosa uaminifu, alikuwa mlevi na mwenye vurugu.

Alisema kuwa wakati walikuwa katika mahusiano mzozo ungetimbuka kati yake na Martin mara kwa mara hadi wakati mmoja akachoka na kufanya maamuzi ya kuondoka.

"Alikuwa mlevi sana. Akija nyumbani alikuwa ananichapa. Wanawake wangepiga simu usiku. Ndoa yangu haikuwa na amani. Nikipata ujauzito hatukuwa tunaelewana nilikuwa naenda kuushughulikia nyumbani na watoto wangu" Esther alisema.

Esther pia alifichua kuwa katika kipindi cha miaka sita ambacho hawajakuwa pamoja na mume huyo wake wa zamani hajawahi kushughulikia watoto kamwe.

Esther alidhihirisha wazi kuwa hakuna uwezekano wake  kurudiana na Martin kwa kuwa tayari ameolewa na mwanaume  mwingine.