'Aliniacha na mtoto mchanga sana akatoroka,'Mwanamke amwanika mumewe

Muhtasari
  • Siku ya Ijumaa bwana Levy allituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake ambaye alidai kwamba amekuwa akinuna kila siku nyumbani
Gidi na Ghost asubuhi
Gidi na Ghost asubuhi
Image: RADIO JAMBO

Siku ya Ijumaa bwana Levy allituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake ambaye alidai kwamba amekuwa akinuna kila siku nyumbani.

"Naomba nipatanishwe na mke wangu, ambaye amekuwa akinuna nyumbani bila ya kuniambia sababu ya kununa, naona anashuku kwamba nina mpango wa kando lakini sina

Pia nikiongea na mtu kwa simu anadhani naongea na mwanamke,mimi sio mlevi wala sina mpango wa kando."

Baada ya kumfikia mkewe, Mama Ibrah alisema kwamba mumewe alimtoroka na kumuacha.

"Sijui kwa nini amenipeleka kwa Radio na ni yeye alinitoroka na kuniambia kwamba anaenda kazi aliniacha na mtoto mdogo ambaye ananyonya

Arudi nyumbani ili tuweze kuongea,"Alisema mkewe Levy.

Kwa mengi zaidi tembelea Radio Jambo Youtube.