"Nilijionea na macho!" Mwanadada asimulia alivyomfumania mumewe na mpango wa kando

Muhtasari

•Eric alisema mkewe alifika majogoo na kumkuta kama bado yupo kitandani na yule mpango wake wa kando.

•Kerubo alisema kuwa hana kinyongo chochote dhidi ya mumewe na kudokeza dalili za kurudiana naye.

Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi Eric Uhuru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Janet Kerubo ambaye alimuacha baada ya kumfumania na mapngo wa kando.

Eric alisema mkewe alikuwa ameenda kwao baada ya kuzozana kidogo wakati aliamua kuleta mwanadada mwingine nyumbani. Alisema majirani walimfikishia mkewe taarifa na hapo akapiga hatua ya kurejea nyumbani  kujithibitishia mwenyewe.

Eric alisema mkewe alifika majogoo na kumkuta kama bado yupo kitandani na yule mpango wake wa kando.

"Tumekuwa tukikosana kidogokidogo. Alijua nilikuwa na mpango wa kando. Nilikuwa napigiwa simu alafu naenda kuchukulia nje. Wakati mwingine  niligiwa simu alafu anachukua.

Kuna wakati alikuwa amenifumania na mrembo kwa nyumba. Tulikuwa tumekosana alafu akaenda kwao nikaleta mwanadada kwa nyumba. Majirani walimpigia simu wakamwambia wameniona na  mwadada mwingine.

Asubuhi kuamka nilimpata akiwa amesimama kwa mlango. Mrembo alikuwa ndani ya nyumba. Tulijaribu kusuluhisha lakini hakuelewa. Huyo mwanadada alitoroka akaenda ," Eric alisimulia.

Eric alieleza kuwa amekuwa kwa ndoa na Kerubo kwa takriban mwongo mmoja. Alifichua kuwa walijitosa kwenye ndoa baada ya Kerubo kushika mimba akiwa na umri wa miaka 16.

Kerubo alipopigiwa simu alisita kukubali msamaha wa mumewe huku akieleza hofu kuwa Eric tayari yupo kwenye ndoa nyingine.

Alifichua kuwa mwanadada ambaye mumewe alijitosa kwenye ndoa naye baada yao kutengana amekuwa akimtumia meseji za matusi.

Nitakusamehea aje na uko na bibi mwingine? Mliachana aje  na yeye na ananitusi? Ananiandikia meseji akinitusi. Anasema wewe ndio ulimwambia anitusi. Mimi sijawahi kuwaandikia meseji. Lakini yeye huwa ananiambia ati mko na yeye na unamwambia anitusi," Kerubo alimwambia Eric.

Kerubo alithibitisha kuwa alimfumania mumewe na mpango wake wa kando ndiposa akaamua kugura ndoa yao.

"Nilijionea na macho. Nilijionea mwenyewe. Ilikuwa saa mbili asubuhi. Nilipata wamelala ata hawajaamka. Nami niko tu nang'ang'ana na watoto. Mi napambana tu na maisha. Sijawahi pigia huyo msichana simu na sijawahi kumpigia simu," Alisema.

Eric alimuomba mkewe msamaha huku akisisitiza kuwa tayari ametengana na mwanadada aliyekuwa anachumbia.

"Naomba tu arudi. Huyo mtoto hayuko na mimi," Alisema.

Kerubo alisema kuwa hana kinyongo chochote dhidi ya mumewe na kudokeza dalili za kurudiana naye.