Sio kila siku mwanaume akirudi kwa nyumba itakuwa baby baby, honey- Gidi amshauri mwanadada

Mercy alisema mumewe alimwagiza atoke kwake kwa kukosa kumuamini.

Muhtasari

•Mercy alisema kwamba  mumewe alimshtumu kwa kukosa kumwamini na kumwagiza aondoke kwa boma yake.

•Gidi alimshauri Mercy aweze kumuelewa mumewe iwapo angependa ndoa yao iwe na amani.

Ghost Mulee na Gidi Ogidi
Ghost Mulee na Gidi Ogidi
Image: RADIO JAMBO

Mercy Ahisia ,24, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Joseph Were ,32, ambaye aligombana naye Jumanne jioni.

Alisema mambo yaligeuka kuwa ya mabaya baada ya kumuuliza mumewe kuhusu alikokuwa akitoka usiku sana.

Mercy alisema kwamba  mumewe alimshtumu kwa kukosa kumuamini na kumwagiza aondoke kwa boma yake.

"Mzee alirudi jana usiku saa tatu. Aliniambia alikuwa kuosha pikipiki, sikuamini.  Alipigia rafiki yake akathibitisha kuwa kweli alikuwa kuosha  pikipiki. Nilimuuliza ni lini tena aliwahi kurudi usiku akasema kama namshuku niende," Mercy alisema.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa kwa mwaka mmoja.

Mercy alisema alikosa kumuomba mumewe msamaha licha ya yaliyotokea kwa kuwa wote wawili ni vichwa ngumu.

"Yeye ni kichwa ngumu na pia mimi ni kichwa ngumu. Mimi sikumuamini. Vile alipigia rafiki yake niliamini na ndiposa nataka kuomba msamaha," Alisema.

Were alikata simu punde baada ya Gidi kumuelekeza Mercy aombe msamaha. Hata hivyo ilisikika kama alikuwa kazini.

Gidi alichukua fursa hiyo kumshauri Mercy aweze kumuelewa  mumewe na hali ya kazi yake iwapo angependa ndoa yao iwe na amani.

"Wewe unafikiria mwanaume akirudi kwa nyumba kila siku ni baby baby, honey. Lazima uelewe wakati mwingine atakuja akiwa amechoka," Gidi alimwambia Mercy.

"Leo jioni umtayarishie chakula, umkaribishe vizuri kisha umuombe msamaha," Aliongeza.

Mercy pia alishauriwa aweze kuwa mvumilivu katika ndoa yake.