Patanisho: "Tunalala kama kondoo!" Jamaa amlalamikia mkewe kwa kutompikia Omena

Peter alieleza kuwa mkewe amekuwa akimshuku kuwa na mpango wa kando baada ya kukataa chakula alichopika.

Muhtasari

•Peter alisema kuwa ingawa bado hajatengana na mke wake, hakujakuwa na amani kwa boma yao kwa muda mrefu.

•Peter alilalamika kuhusu hatua ya mkewe kupika mchele mara kwa mara na kukosa kumpikia Omena.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi ktengo cha Patanisho, Peter alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Wambui.

Peter alisema kuwa ingawa bado hajatengana na mke wake, hakujakuwa na amani kwa boma yao kwa muda mrefu.

Alieleza kuwa Wambui amekuwa akilalamika kila wakati na  kumshuku kwa kuwa na mipango ya kando.

"Wakati nimetoka kazi nikiwa nimechoka nanyamaza kupumzika na kidogo, bibi anauliza nimetoka wapu. Wakati huo nimechoka hata sijiskii kukula anauliza kwani nimepata bibi mwingine na kula huko?!' Peter alisema.

Aliongeza, "Tunalala kama kondoo na  hii baridi! Sio kusema sileti chakula kwa nyumba eti analala njaa. Hata hajawahi kunipaa na mpango wa kando. Yeye ni kunishuku tu. Ni mambo ya kuambiwa. Wakati mwingine simu haishiki kwa nyumba, nikitoka nje kutafuta network anasema eti nimeenda kuongea na wanawake wengine. Bado tuko na yeye lakini hakuna amani kwa nyumba."

Wambui alipopigiwa simu alidai kuwa mumewe amekuwa akimkasirikia mara kwa mara bila sababu zozote.

Alisisitiza kuwa Peter yuko na mahusiano ya nje na kuweka wazi kuwa hata amekuwa akipanga kumuacha.

"Akikuja kwa yumba, kazi yake ni kushinda amenikasirikia. Mimi ata nimepanga nitafute kazi mbali nimuondokee. Ako na wanawake. Ni mwanaume yupi mnakaa na yeye wiki mbili na hata hamlali pamoja?!" Alisema.

"Huwa anaenda kuongea na simu kama amejificha nisisikie"

Peter alisisitiza kuwa madai ya mpango wa kando hayana msingi wowote na kubainisha kuwa mkewe anashuku mambo yasiyo na ukweli wowote.

Alilalamika kuhusu hatua ya mkewe kupika mchele mara kwa mara na kukosa kumpikia Omena ambacho ni chakula akipendacho.

"Nimeshinda nikikula mchele kila wakati.Nilinunua Omena na inaharibikia kwa nyumba. Siwezi kula mchele kula siku.  Anapika chakula yenye sikuli. Nimemfunza hata kupika chakula zote," Alisema.

Wambui alihoji, "Tunawezaje kuwa tunakula omena kila siku? Anapenda hiyo lakini siwezi kupika kila siku."

Wambui alisema kuwa hapendi kula omena na kusisitiza kuwa anapenda kubadilisha chakula anachopika kwa nyumba.

"Mimi sina mambo mingi, yeye ndiye ananionyesha madharau. Mimi siwezi kupika ugali kila siku. Huwa napenda kubadilisha. Mimi ata sipendi Omena," Alisema Wambui.

Wawili hao walikubaliana kushiriki kikao baadae ili kusuluhisha mzozo kati yao.