Patanisho: "Unatumaje 100 alafu unareverse!" Mwanadada amfokea aliyekuwa mumewe

"Achana na mimi. Tulimalizana na wewe. Hakuna vile tunaweza kurudiana," alimwambia.

Muhtasari

•Ndungu alidai kwamba mzazi huyo mwenzake aligura mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya kuzozana naye na kuchochewa na dada zake.

•Esther pia alidai mumewe hakuwa akiwajibikia majukumu mengi ya nyumbani.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Joseph Ndungu ,33, alituma ujumbe akiomba ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mke wake Esther Wambui ambaye alimuacha mwaka jana.

Ndungu alidai kwamba mzazi huyo mwenzake aligura mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya kuzozana naye na kuchochewa na dada zake.

"Nilikuwa nimeoa bibi miaka miwili. Alikuwa anakuja saa tano usiku kutoka kazi. Siku zingine nikimuuliza anakasirika. Alitoroka alafu tukaongea akarudi.  Tuliporudiana, dada yake akaja kukaa kwetu. Nikakubali akae ili awe anakaa na mtoto wetu," alisimulia.

Ndungu alisema kuwa kukaa kwa shemeji yake hakukuwa kuzuri kwani alikuwa akifanya makosa pale nyumbani.

"Nikimkosoa, mke wangu akawa anaegemea upande wake. Siku moja niktoka kazini nilikuta wametoroka. Walikuwa wameitana dada wote watatu, kumbe walikuwa wanapanga kutoroka. Nilikuta wameenda wote na kubeba vitu vya nyumba," alisema.

Alisema kwamba juhudi zote ambazo ameweka za kupatana na Esther hazijafua dafu. Mke huyo wake wa zamani pia hajakuwa akichukua simu zake.

"Watu wa kwao wanaegemea upande wake. Wazazi wake bado hatujaongea"

Esther alipopigiwa simu alimtaka mumewe huyo wa zamani kuachana naye huku akimbainishia kwamba hakuna uwezekano wa kurudiana.

"Achana na mimi. Tulimalizana na wewe. Hakuna vile tunaweza kurudiana," alimwambia.

Aliendelea kufichua jinsi Ndungu hajakuwa akiwajibikia majukumu yake kama mzazi.

"Kuna siku ulituma pesa alafu ukareverse. Mia moja alafu tu ukatoa!!Soo moja alafu unareverse, si ingekuwa ngiri. Mia inaweza kununua nini?" alisema.

Esther pia alidai mumewe alikuwa mvivu na alimuacha kugharamia mahitaji mengi ya nyumbani.

"Kuna kitu ilikuwa inaniuma. Akienda kazi ya boda alikuwa anarudi kwa nyumba analala alafu anatoka saa kumi na moja, akirudi hana pesa. Mimi ndio nilikuwa nalipa nyumba. Alikuwa anakuja na mia mbili," alisema.

"Ilikuwa inafika mahali anaanza kuongea vibaya. Ilikuwa ni mazoea. Nilichoka nikaenda,"

Mama huyo wa watoto wawili aliweka wazi kwamba tayari amesonga na maisha yake na kumuomba Ndungu aache kumfuatilia.

Ndungu hata hivyo alimtaka ampatie watoto wao huku akimuonya wasiwahi kulelewa na mwanaume mwingine.

"Watoto wangu wasiwahi kulelewa na wanaume wengine. Hiyo ni mambo ya uongo ambayo amesema. Usizungushe damu yangu!" alisema.

Je, ushauri wako ni upi kwa wanandoa hao wa zamani?