Patanisho: Jamaa apata mkewe ametoroka baada ya kuenda matanga ya binamuye

"Kabla aende alikuwa akisema anashuku niko na mpango wa kando," Mavia alisema.

Muhtasari

•Mavia alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka miwili wakati alipokuwa ameenda nyumbani kwa ajili ya matanga ya binamu yake.

•Everlyne alipopigiwa simu alikana kumjua Mavia kabla ya kukata simu.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Alhamisi asubuhi, Baldwin Mavia Bebetu ,29, kutoka Kawangware aliomba kupatanishwa na aliyekuwa mke wake Everlyne Viyai.

Mavia alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka miwili wakati alipokuwa ameenda nyumbani kwa ajili ya matanga ya binamu yake.

"Wakati nilienda Kitale kwa matanga ya binamu yangu. Kurudi nilipata amebeba vitu na watoto wetu wawili ametoka kwa nyumba.Aliondoka na watoto wake wawili na kuacha yule wangu mmoja. Hatukukosana," alisema.

Aliongeza, "Nimekuwa nikimpigia simu arudi lakini hajawahi kuja. Sijaenda kwa dadake kujua ako namna gani."

Mavia alidokeza kwamba kabla ya mkewe kuondoka alishuku kuwa anaenda nje ya ndoa yao.

"Kabla aende alikuwa akisema anashuku niko na mpango wa kando. Sikuwa naye, alikuwa anashuku tu.Kuna mwanamke ambaye nilikuwa naye alienda kabla yake. Alikuwa anadhani tunazungumza naye lakini ni fitina za ploti," alisema.

Everlyne alipopigiwa simu alikana kumjua Mavia kabla ya kukata simu.

"Simjui!" alisema.

Mavia alisema, "Hajawahi kueleza shida yoyote. Tumeongea hadi na mchungaji akiulizwa shida ni nini lakini hajaeleza."

  1. Kufuatia hayo, alitumia fursa yake hewani kumsihi mzazi huyo mwenzake kurudi ili waendeleze familia naye.

"Mama Fayee mahali ulipo, naomba urudi tukae pamoja tuendelee na shughuli yetu ya mbele. Njoo tujengee watoto. Kwa yale nimekosea, naomba unisamehe. kama kuna mabaya, tutaongea mbele ya wazazi," alisema.

Je, una ushauri gani kwa Mavia?