Patanisho: Mpango wa kando amtumia mke wa mpenziwe mazungumzo yao na picha ya uchi

"Niko na mipango wa kando watatu. Wa mwisho ndiye amechoma, alichukua picha yake akatumia mke wangu alafu akanifowardia." Simiyu alisema.

Muhtasari

•Simiyu alisema ndoa yake ya miaka minne ilianza kusambaratika mwezi jana baada ya mkewe kugundua anaenda nje ya ndoa.

•Moureen alilalamika kwamba mumewe alimpost mpango wa kando kwenye Facebook ila hajawahi kumpost yeye.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Jumanne asubuhi, Alex Simiyu (27) kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Moureen Wanjala (29) ambaye alikosana naye mwezi uliopita.

Simiyu alisema ndoa yake ya miaka minne ilianza kusambaratika mwezi jana baada ya mkewe kugundua anaenda nje ya ndoa.

"Tunaishi na mke wangu Mombasa. Kuna wakati nilimdanganya bosi wangu amenituma nimpelekee gari Nairobi. Lakini nilikuwa naenda kwa mpango wa kando. Wakati wa kurudi, mpango wa kando alikuwa ameweka kifaa cha kujipondoa  kwa mkoba wangu, sikujua. Bibi yangu alipofungua begi akaipata," Simiyu alisimulia.

Aliongeza "Juzi nilikuwa na mwanamke mwingine mpango wa kando. Niko na mipango wa kando watatu. Wawili tu ndio nimeona. Wa mwisho ndiye amechoma, alichukua picha yake akatumia mke wangu alafu akanifowardia."

Simiyu alisema mkewe na mpenziwe walikuwa wakiwasiliana kwenye mtandao wa Facebook ambapo mpango huyo wa kando alimfichulia mengi kuhusu uhusiano wao na hata kumtumia picha.

"Sasa yuko (mkewe) kwa nyumba lakini hatuzungumzi," alisema.

Moureen alipopigiwa simu alifichua kwamba mumewe amekuwa na mahusiano ya kando mara kwa mara licha ya kuwa kwenye ndoa.

"Si mara ya kwanza, amezoea kufanya hivyo. Sasa hatuongei, yeye ndiye mwenye makosa lakini amenyamaza eti mimi nianze kumuongelesha," Moureen alisema.

Simiyu alikiri kujuta makosa yake na kumuomba msamaha mkewe.

"Nimekaa nikifikiria ndio maana nimepeleka Radio Jambo. Nimeamua nataka kutunza familia yangu. Nimeamua nitatulia tulee watoto wetu," alisema.

Moureen alilalamika kwamba mumewe alimpost mpango wake kando kwenye mtandao wa Facebook, jambo ambalo lilimkasirisha na akachukua hatua ya kumtafuta mwanadada huyo hadi wakaanza kuwasiliana.

"Msichana wa nje anampost mitandaoni lakini mimi mke wake hawezi kumpost.Mimi nilimtafuta msichana ambaye alikuwa amepost na tukazungumza. Msichana aliniambia alipogundua ana familia alimtema. Yeye (Simiyu) hakujua naongea na msichana huyo," Moureen alisimulia.

"Kuna wakati msichana huyo alipiga simu akasikia mtoto akiongea alafu (Simiyu) akasema mtoto ni wa jirani.  Huyo msichana alikuwa ananitumia jumbe na mazungumzo yao yote. Shida yake ni mipango wa kando," alisema.

Simiyu alimnyenyekea mkewe na kumuomba radhi kwa makosa yake yote huku akibainisha kuwa ataumia sana akimpoteza.

"Nakupenda kama mke wangu na niko tayari kulinda familia yangu. Nimekiri mbele ya Mungu sitakuwa na mipango wa kando," Simiyu alisema.

Moureen alisema, "Nimemsamehe lakini abadilike tabia. Sio kuwa kama mwanaume ambaye ameoa."

Aliongeza, "Maisha yangu niliamua kukaa kwa ndoa. Mimi nakupenda na ata wewe unajua nakupenda na natamani kuishi nawe maisha yote."

Je, una ushauri gani kwa wanandoa hao?