NDOA YENYE UTATA

Patanisho:Mwanadada wa 28 ajipata katika msukosuko wa ndoa na mzee wa 56

Amekuwa haniruhusu hata kutembea, hata simu yangu ikipigwa anasema ni mwanaume mwingine amenipigia

Muhtasari

•Wewe ndiwe ulienda. ulisema unaenda kanisani ukaenda kabisa. mimi nimeangalia njia sikuoni mamaa. Sina shidsa nawe nataka urudi nyumbani ulee mtoto wako. ni wewe ulitoka.

•Hata namba yake sina, nilikuwa nayo ikapotea, labda yeye anipigie ili iingie. 

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

PATANISHO: Katika kitengo cha patanisho, Rose Nanjala ameomba kupatanishwa na bwanake John Chemiak, waliodumu katika ndoa kwa miaka 6 wakijaliwa na mtoto mmoja. Anakiri kukosana na John kwa kumzingizia kuwa na mwanaume mwingine nje ya Ndoa.

“Hello Jambo mimi ni Rose Nanjala 28yrs kutoka Tulienge, Bungoma County. Naomba kupatanishwa na Baba Mtoto na Bwana yangu anaitwa John Chemiak 56yrs. Tumekuwa kwa ndoa kwa miaka sita na tuko na Mtoto moja. Nilikosana na Bwana yangu on Feb 2023 baada ya yeye kunisingia eti niko na wanaume nje. Kwa hivi sasa niko kwa Dada yangu hapa Nairobi na yeye ako kule Bungoma.”

Kulingana na maelezo ya Nanjala, wamekuwa wakiishi vizuri, ila sitofahamu za mumewe zikaendelea kuzidi. Ameeleza kuwa hata akipigiwa simu bwanake anashuku kuwa huenda amepigiwa na bwanake mwingine. Anadai kughadhabishwa na tabia hiyo iliyochangia kuondoka bado akiwa angali na ujauzito, akaenda kujifungulia nyumbani. 

Licha ya hayo, Nanjala, 28,  ameeleza kuwa bwanake alikwenda kumchukua mtoto kilichochangia kuandamana naye tena japokuwa miaka miwili baadaye alitoroka tena.

“ Tumekaa tu vizuri, simu ikipigwa anasema huyo ni bwanako, hataki hata utembee. Alinipatia ujauzito ikabibi nitoke niende kwetu nikajifungue. Amekuja tukaongea, nikarudi lakini kurudi pia tarizo ni lilelile. Alikuja nyumbani akachukua mtoto, nikamfuata halafu bado tatizo ni lile lile. Halafu sasa nikatoka nikaenda sasa kwa sister yangu. Miaka si haja. hata kama miaka yake ni yangu maradufu. Ni mara ya tano kujaribu kurudi tuishi pamoja maana bado nampenda.”

Kulingana na John, amedai kuwa yeye hana shida na mpenziwe. Anasema kuwa ni yeye aliondoka kwa madai ya kwenda kanisani na tangu hapo hajawahi kurudi. Amekiri angali anampenda na yupo tayari kumpokea wakati wowote atakapojihisi kurejea.

Wewe ndiwe ulienda. ulisema unaenda kanisani ukaenda kabisa. mimi nimeangalia njia sikuoni mamaa. Sina shidsa nawe nataka urudi nyumbani ulee mtoto wako. ni wewe ulitoka.Mimi sina makosa na yeye, hata yeye anajua nilimwoa tukapata mtoto lakini baadaye akaenda. Baada ya miaka miwili akarudi, akakaa tena akaondoka. Amekaa sana akaondoka. Akasema yeye anaenda kumwomba Mungu hata nikampa nauli. Sasa anataka kurudi tena. Mimi sina shidsa naye, niko tayari kumpokea. ” Alisimulia bwana John.

Hata hivyo, John, 56,  anasema kuwa mawasiliano hayajakuwa yakifanyika maana nambari ya simu ya mpenziwe ilipotea, akidai kuwa ni hadi ampigie ndipo aweze kuipata tena.“Hata namba yake sina, nilikuwa nayo ikapotea, labda yeye anipigie ili iingie. ”

Ungetoa ushauri upi kwa wapenzi hawa wali?