Stress niko nazo naelekea kufa, kifo tu ndo naona mbele yangu!-- Mwanadada amlilia ex wake

Nelson alilalamikia tabia ya mkewe ya kuhamahama na kupost wapenzi wake wa zamani.

Muhtasari

•Moraa alisisitiza kwamba alitaka tu kujua msimamo wa Nelson na kubainisha amekumbwa na msongo wa mawazo.

• "Endelea na maisha yako uishi, mimi nishamove on. Usione shida ukanikumbuka. Kama hukuwa wangu kuna mwenye Mungu amekuwekea. Hiyo mambo ya mimba sijui," Nelson alisema.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Mercy Moraa ,26, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Nelson Ochonga ,26, ambaye alikosana naye mwezi moja uliopita.

Moraa ambaye aliweka wazi kwamba kwa sasa ana ujauzito wa Nelson wa miezi minne alisema mumewe aliondoka nyumbani mwezi uliopita akidai kwamba ameenda kuangalia maharage nyumbani.

Alisema baada ya mumewe kuondoka alienda na kuoa mwanamke mwingine ambaye alitafutiwa na dada zake.

"Tulikuwa tunaishi na yeye nyumbani. Juu ya kelele ya mama mkwe nikamwambia tutoke. Akakubali tukatoka tukaenda Narok. Alilipa nyumba tukakaa mwezi moja. Alisema ameenda nyumbani kuona maharage. Alisema ameenda atarudi. Niliporudi kwa nyumba nilipata ni watoto tu wako yeye ameenda," Moraa alisimulia.

Aliongeza, "Alienda na kila kitu hadi nguo chafu. Kumuuliza alisema nguo anaweza kurudi nazo. Alikuwa amesema atarudi Jumamosi iliyokuwa inafuata. Kabla ya Jumamosi, niliambiwa kwamba dada zake wamemletea bibi mwenye ako na mtoto mmoja. Juzi alinipigia simu akaniambia bado tuko pamoja."

Alisema kuwa shangazi wake ambao wanaishi karibu na kwa kina Nelson ndio waliompa taarifa kuhusu hatua ya mpenziwe huyo kuoa.

"Dada zake pia waliwapiga picha wakaweka Facebook. Ningetaka kujua msimamo wake. Niko na mimba ya miezi minne,  Anajua." alisema.

Nelson alipopigiwa simu alikiri kwamba tayari ameendelea na maisha yake na kudokeza baadhi ya sababu zilizochangia yeye kumtema Moraa.

"Huyo mwanadada alinikosea sana nikaona nikuje nyumbani. Mambo ya kuhamahama anatoka anaenda, nilichoka. Huyo msichana tumetoka naye mbali lakini kuna mambo nimesikia. Nimempigia simu jana akaniambia kwaheri eti ameenda kwa mwanaume mwingine. Mnamo siku ya kina baba alipost   ex wake . Hiyo inauma. Nilikuja nyumbani mwezi jana nikakuja nikamove on, nikaona," Nelson alielezea.

Moraa alisisitiza kwamba alitaka tu kujua msimamo wa Nelson na kubainisha amekumbwa na msongo wa mawazo.

"Nilikuwa nataka nijue msimamo wako kwa sababu nimekuongelesha siku nyingi na unasema tu utarudi. Stress niko nazo naelekea kufa, kifo tu ndo naona mbele yangu kwa sababu nakupenda," alisema Moraa.

Nelson alisema, "Kama nishamove on ata wewe si uende kwa mwanaume mwingine. Si uende kwa mwenye ulisema uko naye. Kwa nini unapost picha zangu na nishamove on." 

Alipoulizwa kuhusu mimba ambayo Moraa anabeba, alisema "Hapo mimi sitakujibu. Zaa ndio tuone tutafanya aje kama uko na mimba."

Alisisitiza kwamba kabla ya kufanya uamuzi wa kuondoka walijaribu kusuluhisha mzozo wao ila Moraa hakuwahi kubadilika.

"Na hiyo nini anapost ati ako na Father's day anapost wanaume, kitu kama hiyo utakaa naye aje??" alihoji.

Moraa alijitetea, "Nilipost hiyo siku auntie zangu waliniambia ameletewa wanaume. Nilikuwa na hasira nikaona nipost. Alinipost nikamuelezea. Ata yeye anajua hakuna mwanaume najua napenda kama yeye. Nitakaa tu kama single mother hakuna mwanaume mwingine naweza kupenda kama yeye."

Maneno ya mwisho ya Nelson kwa Moraa yalikuwa, "Endelea na maisha yako uishi, mimi nishamove on. Usione shida ukanikumbuka. Kama hukuwa wangu kuna mwenye Mungu amekuwekea. Hiyo mambo ya mimba sijui. Sikuwahi kujua. Hatujawahi kuenda kupima ujauzito. Atazaa tu tutalea mtoto."

Moraa alimwambia Nelson, "Wewe kama umemove on ni sawa lakini jua tu nakupenda. Hivi karibuni nitakuwa na mtoto wako. Wewe ndo utajua vile utafanya na mtoto wako."

Je, una ushauri gani kwa wawili hao?