logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mke akataa kuishi na mumewe Murang'a, alalamika kuna baridi kali

Kevin alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilisambaratika mwishoni mwa mwaka jana baada ya mkewe kukataa kuenda kuishi naye.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi29 January 2024 - 06:19

Muhtasari


  • •Kevin alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilisambaratika mwishoni mwa mwaka jana baada ya mkewe kukataa kuenda kuishi naye.
  • •Kevin ambaye alisikika kusikitika alisema, "Wacha akae. Kama hataki hii baridi, mimi siwezi toka kwa kazi yangu niende Nairobi."

Raia wa Uganda ambaye alijitambulisha kama Kevin Simeraa ,27, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Miriam Isuku ,28, ambaye pia ni raia wa nchi hiyo jirani.

Kevin ambaye anafanya kazi katika eneo la Kandara, kaunti ya Murang'a alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilisambaratika mwishoni mwa mwaka jana baada ya mkewe kukataa kuenda kuishi naye.

"Mke wangu tumekaa naye mwaka mmoja. Nafanya kazi Muranga, yeye ako Nairobi. Disemba 2023 alisema nimpatie nauli aende kwao. Akiwa kwao alisema nimtumie nauli arudi. Nilimwambia bosi ako mbali atafute nauli nitamrudishia. Alisema kama ni hivyo atafute kazi ingine hatawezana na hiyo," Kevin alisimulia.

Kevin alifichua kwamba mkewe alipinga ombi lake la kuenda kuishi naye Murang'a huku akidai kwamba kuna baridi sana.

"Nilimwambia akuje akasema hapana. Alisema kama nataka niache kazi niende tuishi Nairobi. Anataka niache kazi niende tuishi Nairobi. Nashindwa tutalipa kodi na nini. Anasema Murang'a baridi ni mingi," Kevin alisema.

Aliongeza, "Yeye anafanya kazi ya nyumba. Mimi nalisha nguruwe na ng'ombe. Bado sijaenda kwao. Tulipatana Uganda. Watu wao wananijua sana. Nataka nijue msimamo wake kwani mawazo yangu yote nimempatie yeye."

Juhudi za kuwapatanisha wawili hao hata hivyo iligonga mwamba kwani Miriam hakuweza kupatikana kwa simu.

Kevin ambaye alisikika kusikitika alisema, "Wacha akae. Kama hataki hii baridi, mimi siwezi toka kwa kazi yangu niende Nairobi."

Aliongeza, "Akuje tukae hapa Muranga tuzoee baridi ya Muranga juu ata kwetu kuna baridi nyingi. Nitamnunulia kila kitu anataka."

Je, una maoni yapi kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved