Patanisho: Jamaa mwenye mke na watoto 3 atongoza msichana na binamu yake

"Nilikuja kujua ako na familia. Ako na watoto wanne na bibi Mkikuyu," Joy alilamika.

Muhtasari

•Wilson alisema mahusiano yao ya miaka miwili yalisambaratika mwaka wa 2022 kufuatia suala la kukosa uaminifu katika ndoa.

•Joy alipopigiwa simu alithibitisha kwamba mpenzi huyo wake wa zamani alimtongoza binamu yake na hata kumtunga mimba.

Gidi na Ghost studioni
Image: RADIO JAMBO

Wilson Mireri ,32, kutoka Githurai alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mpenzi wake, Joy Kerubo (23) ambaye alikosana naye takriban  miaka miwili iliyopita.

Wilson alisema mahusiano yao ya miaka miwili yalisambaratika mwaka wa 2022 kufuatia suala la kukosa uaminifu katika ndoa.

Alimshtumu mpenziwe kwa kuwa na mpango wa kando.

"Yeye alikuwa na mpango wa kando. Alikuwa akiniambia anaenda kwao, namruhusu. Akifika huko anaenda kwa mpango wa kando. Alifika huko kwao nikamwambia siku yenye atarudi Nairobi nitampanga, hakurudi.

Nikauliza mama yake akaniambia anaenda kwa nyanya yake. Baadaye niliuliza marafiki nikaambiwa msichana ambaye nilikuwa nimeoa ameonekana. Nilitoka Nairobi nikaneda mpaka Kisii, kweli nikampata huko," Wilson alisimulia.

Aliongeza, "Mama yake alienda wakaongea, tukarudiana. Akaja Nairobi, baada ya muda alianza kuzungumza na huyo mpango wa kando. Vile alinionyesha madharau nilianza kutongoza binamu yake. Vile alisikia alikasirika. Nataka kumuomba msamaha kama ni kurudiana turudiane. Binamu yake tuliachana na yeye."

Alidai kwamba jamaa ambaye mpenziwe alijitosa katika mahusiano naye alikuwa ni rafiki yake.

Joy alipopigiwa simu alithibitisha kwamba mpenzi huyo wake wa zamani alimtongoza binamu yake na hata kumtunga mimba.

"Mwambie akuje atafute binamu yangu mwenye alikuwa analala. Ata ako na mtoto mdogo naye. Binamu yangu ako na HIV/AIDS, aniache kwa amani. Huyo kijana ata sitakangi kusikia sauti yake," Joy alisema.

Aliongeza, "Wakati alianza kuchumbiana na binamu yangu ndio ata mimi nilipata mpenzi. Ata ni marafiki zangu waliniambia sikuwa najua. Niliambiwa niangalie mtandao, nikapata amepost binamu yangu. Walikuwa wanakunywa pombe pamoja.Mwambie aniache kwa amani. Hizo simu ananipoigia eti ananiota, mimi sio mchawi aniache kwa amani."

Joy pia aliibua madai kwamba mpenzi huyo wake wa zamani alikuwa na familia nyingine.

"Nilikuja kujua ako na familia. Ako na watoto wanne na bibi Mkikuyu. Binamu yangu alikuwa anachapwa na wamama Wakikuyu. Hapo ndo nilijua alikuwa na bibi na watoto," Joy alisema.

Wilson alisema,  "Nilikuwa nataka tu kuomba msamaha juu hiyo kitu ya kuchukua binamu yake ilileta shida kwa familia yake. Anisamehe. Pia aambie mama yake anisamehe."

Pia alikiri kuwa na watoto na aliyekuwa mpenzi wake.

"Chenye wasichana wamenionyesha ni mengi na ata sina haraka ya kupata mwingine. Ata nilikuwa na mwanamke mwingine Mkikuyu. Tulipata watoto watatu. Nilimnyang'anya kijana akaenda na wasichana.Wazazi walikuwa wananisukuma nipate bibi kutoka kwa kabila yangu, ndipo nikapata Joy," alisema.

Joy alisema, "Mimi nimemsamehe lakini aache kunipigia simu niko na bwana na mtoto."

Je, una maoni au ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?