Patanisho:Mwanadada akiri kuwa muongo na kusamehewa na mumewe

Paul Munene ,34 alimsamehe mpenzi wake Sofia,26 na kudai kuwa yeye amevunjwa roho na wasichana wengi huku Sofia akikubali kurekebisha tabia zake za uongo.

Muhtasari

•Sofia alisema kuwa alikosana na mpenzi wake Paul Munene kwa kutohudhuria mazishi ya mama mzazi wa mpenzi wake.

•Paul alipopigiwa simu alidai kuwa Sofia amekuwa akimdanganya kwa siku mingi,wakipanga kukutana hatokei ilhali yeye alikuwa anampenda sana.

•Sofia alikubali kurekebisha tabia zake na  kusema kuwa atampenda mno bwana Paul Munene.

GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

 Sofia,26 kutoka Voi alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake ,Paul Munene, 34 ambaye kwa sasa anaishi Nairobi baada ya kukosana wiki tatu hivi majuzi.

Sofia alisema kuwa walikuwa kwa uhusiano na mpenzi wake kwa takriban mwaka mmoja na kukosana hivi majuzi kwa kutoenda  mazishi ya mama mzazi wa mpenzi wake.

"Nilikuwa sawa wakati nilikuwa huku Nairobi,vile shule zilifunguliwa nikarudi Voi kwa kuwa mimi ni mwalimu wa Sekondari.Bwanangu alinipigia simu kuniambia mama yake alikuwa mgonjwa ,nimtumie Ksh.500,nikamwambia sina.Baada ya masaa machache akaniambia mum ashatuacha na sikuenda hio mazishi.Hio ndo ilimkasirisha."

Sofia alidai kuwa hakuwa na pesa ya kusafiri kuelekea kwa matanga.

"Niljaribu kutafuta nauli kutoka kwa watu lakini kila mtu alisema hana.Nikaambia mpenzi wangu kuwa nimekosa nauli na pia mshahara haijafika."

Sofia aliongeza kuwa  akipiga simu bwana yake hujifanya hamjui na kila wakati humuuliza eti ni nani.Wawili hao walikuwa wanapanga kuoana hii mwaka kulingana na Sofia.

Paul alipopigiwa simu alisema kuwa Sofia ameishi akimdanganya kila siku hadi upendo wake ukaisha,akiongeza kuwa hajawahi kumwonyesha madharau hata siku moja.

"Huyo msichana mimi nilikuwa nimejitolea kumpenda yangu yote.Shida ni yeye ananidanganya kila wakati,amefanya niwache wasichana wengi sana,ili nimpende yeye tu.Lakini sasa yeye huwa anajifanya."

Aliongeza; "Tangu tupatane na huyo msichana kwa gari nilikuwa nimevunjwa roho na mpenzi wangu wa kitambo,Sofia venye tulipatana kwa gari,nikaamua kumpa roho yangu na pia yeye akafunguka tukapendana.Aliniambia anafanya kazi hapa side za Umoja nikamwambia sawa ...baaada ya muda mchache akaniambia amehamia Voi.Nilimwambia anisaidie namba ya mamake ,tukaongea na yeye mama yake hana shida.Sofia amekuwa akinidanganya mara ako Embakasi ,mimi simuelewi."

Paul alisisitiza kuwa yeye hana shida na Sofia; "Mimi sina shida na huyo msichana ,mimi ni mtu wa kanisa na ninampenda sana.Yeye awache hizo tabia zake za uongo.NImevunjwa roho na wasichana wengi na hivi nimeamua kukaa na Sophia na kumpenda kwa roho yangu yote.

Aidha,Sofia alisema kuwa yupo tayari kuacha tabia zake za uongo na kumpenda kwa dhati bwana Paul.

Je,una maoni gani kuhusu patanisho ya leo?