Patanisho: Jamaa akasirikiwa na mkewe baada ya kupatikana 'akichat' na ex'

Felix Kiprop amekuwa kwa ndoa na Vilary Jerono kwa miaka 8 na kubarikiwa na mtoto mmoja.

Muhtasari

•Felix aliomba kupatanishwa na mke wake,Vilary baada ya kupatikana  akiongea na mpenzi wake wa zamani kwa facebook.

•Vilary alipogiwa simu alikataa kuombwa msamaha huku akidai sharti waketi chini na kujadiliana jioni ya leo,Julai 1 baada ya kazi.

Gidi na Ghost Studioni
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Felix Kiprop ,30, kutoka Kabarnet alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Vilary Jerono ,29  baada ya kukosana Juni 30,2024.

Felix alisema ndoa yake iliharibika baada ya mke wake kuingia kwenye akaunti yake ya Facebook na kupata kuwa anaongea na wasichana wengine.Wawili hao wamekuwa kwa ndoa takriban miaka 8 na wakabarikiwa na mtoto mmoja.

"Nilikuwa nikiongea na rafiki zangu wa zamani wa shule kule Facebook na nikaacha simu yangu kwa meza kabla ya mke wangu kuichukuwa na kuanza kupekua. Baada ya hapo alinyamaza ghafla na akanikasirikia ,nilijaribu kumuuliza sababu lakini hakuwa ananijibu.Leo asubuhi alienda kazi lakini bado alikuwa amekasirika."

Hata hivyo Kiprop alithibitisha kuwa mke wake aliingia katika akaunti yake ya Facebook na kufuatilia mazungumzo yake.

"Aliniambia kuwa ameingia kwa akaunti yangu na kuona kuwa nilikuwa naongea na wasichana wengine."

Aliongeza, "Sijui ni shetani yupi aliniingilia nikaanza kuongea na wasichana wengine.Nilijaribu kuzuia bibi yangu kutoenda baada ya kumshawishi kwa  maneno.Kuna msichana mmoja tulikuwa 'tunachat' na yeye,alikuwa mpenzi wangu wa zamani.

Vilary alipogiwa simu alikataa msamaha kutoka kwa Felix huku akidai kuwa yupo 'busy' kwa kazi.

"Mimi sitaki kuongelea chochote na sitaki kuombwa msamaha.kufanya kosa si kosa ila kurudia makosa ndiyo balaa zaidi,si mara ya kwanza kumpata akiongea na wasichana wengine..."{alikata simu}

Hata hivyo Felix alisisitiza kumwomba msamaha akidai kuwa kosa laweza samehewa hata mara ya tatu.

"Ningependa tena  kumwomba msamaha kwa mara nyingine mbele ya wakenya milioni ishirini,sitawahi rudia tena..."

Vilary alipigiwa simu kwa mara nyingine na kusema, "Mimi sipo tayari kuongea tena kwa redio,kama anataka aningojee  baadaye na tujadiliane ..."

Je,una maoni gani kwa patanisho ya leo?