"Anashinda kusema sizai, mimi ni tasa niondoke!" Mwanadada akejeliwa na mpenziwe kwa kutozaa

"Tulijaribu kupata mtoto lakini tukashindwa. Nilienda hospitali lakini yeye alikataa kuenda na kuniambia shida ni mimi," Pauline alisema.

Muhtasari

•Pauline alisema ndoa yake ya miaka mitano mnamo Siku ya Wapendanao (Valentine's) mwezi Februari, mwaka huu.

•"Nilianza dating na yeye. Yeye ndiye mpenzi wangu wa kwanza. Huwa naona siwezi kupenda mtoto mwingine vile niko," Pauline alisema.

GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Mwanadada ambaye alijitambulisha kama Pauline Mbete ,22, kutoka kaunti ya Makueni alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Sylvester Kioko ,25, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Pauline alisema ndoa yake ya miaka mitano mnamo Siku ya Wapendanao (Valentine's) mwezi Februari, mwaka huu.

Alisema matatizo katika ndoa yao yalianza kutokana na shida ya kutopata mtoto.

"Tulikuja tukakosana mwezi wa pili. Kila wakati alishinda kuniambia mimi sizai, mimi ni tasa, nitoke alete mke mwingine," Pauline alisimulia.

Aliongeza, "Tena ni mtu mwenye ni vurugu anashinda kunipima. Tulijaribu kupata mtoto lakini tukashindwa. Nilienda hospitali lakini yeye alikataa kuenda na kuniambia shida ni mimi. Nataka turudiane juu nampenda."

Akizungumzia sababu yake kutaka kurudiana na Sylvester licha ya shida zote alizopitia naye, Pauline alisema, "Nilianza dating na yeye. Yeye ndiye mpenzi wangu wa kwanza. Huwa naona siwezi kupenda mtoto mwingine vile niko. Huwa naona kueleza mwanaume mwingine sipati mtoto ni shida.Mimi nampenda tu. Nataka tu turudiane. Lakini akasema hataki ni sawa. Ata juzi alikuwa na matusi mingi mingi."

Pauline pia alizungumza kuhusu hali ya ndoa yao akiweka wazi kuwa mpenziwe hakuwa amemtambulisha nyumbani.

"Hakutaka wazazi wake wajue tuko pamoja. Nilikuwa nimeambia wazazi wangu kwamba naishi na mtu. Wakati nilimsukuma aambie wazazi wake tuko na yeye, hapo ndio shida ilianza," alisema Pauline.

Sylvester alipopigiwa simu, Pauline alichukua fursa hiyo kueleza nia yake ya kurudiana naye.

"Hizo mambo zote tumepitia na wewe ni ngumu kukupoteza. Sasa nilitaka kujua uamuzi wako," alimwambia mpenziwe.

Sylvester alisema, "Mimi sina shida juu maneno. Kama ni kukusamehe naweza kukusamehe tuendelee pamoja. Naweza badilika. Mimi nampenda. Kabla nimtambulishe kwetu, lazima niangalie mambo kadhaa, kama vile atakuwa mwaminifu kwangu. Nitaamua vile nitafanya, nitafanya uamuzi wangu ambao unaweza kueleweka,"

"Pauline, mimi nakupenda. Hii maneno mingi tuachane nayo. Lazima tusonge mbele pamoja," alimwambia mpenziwe.

Pauline alimwambia, "Usikuwe unanilazimisha kufanya mambo. Kama unataka turudi na wewe. Ujue tukae na amani. Sitaki ndoa ya shida."