"Nilijilipa zenye nilikuwa namlisha" Mwanadada afunguka sababu ya kutoroka na vitu za jamaa

"Nilijilipa zenye nilikuwa namlisha. Niliuza nikiwa huko kabla niende Mombasa," Lilian alisema.

Muhtasari

•Derick alisema ndoa yake ya miaka miwili imekuwa na misukosuko na ilisambaratika kabisa wakati mkewe alipotoroka na kubeba baadhi ya vitu vya nyumba.

•"Haja gani uishi na mtu hapendi watoto wako. Wakati sina kazi sitakula, wakati niko na kazi ndo nitakula," Lilian alilalamika.

Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Derrick Ochieng' ,30, kutoka Nairobi alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mke wake Lilian Atieno ,26, ambaye alikosana naye takriban mwezi mmoja uliopita.

Derick alisema ndoa yake ya miaka miwili imekuwa na misukosuko na ilisambaratika kabisa mwezi uliopita wakati mke wake alipotoroka na kubeba baadhi ya vitu vya nyumba.

"Tumekaa na yeye miaka miwili, nilimpata na watoto wawili, msichana na mvulana. Heshima imekosekana, amekuwa akienda namfuata. Pia amekuwa akinishuku na kusikiliza maneno ya watu . Akiambiwa nimefanya kitu anaamini bila kufuatilia. Siku moja nilitoka kazi nikapata amebeba kila kitu akaenda. Aliniblock kwa simu, nikipiga hashiki," Derick alisimulia.

Aliongeza, "Nilitoka asubuhi nikienda kazi. Nikamwambia nitaenda nimtumie pesa ya kuenda hospitali. Jioni nilipata mlango imefungwa. Alienda na TV ya wenyewe.Mwenye TV alinipeleka hadi kwa polisi. Waliniambia nishughulikie. Nimejaribu kufuatilia lakini sijafanikiwa.  Alibeba pia gas na mitungi. Nilimuoa kwa kuwa nilitaka mwenye tunakaa na yeye tunapanga maisha. Nilikuwa nashughulikia hadi watoto wake."

Lilian alipopigiwa simu, aliweka wazi kwamba hawezi kurudiana na jamaa huyo akidai kwamba anaelewa makosa yake.

Alidai kwamba mpenziwe huyo wa zamani amekuwa akiomba msamaha mara kwa mara ila anarudia makosa baada ya kusamehewa.

"I am not your mother please. I am not your baby. Mbona unipeleke kwa radio na unajua shida yako. Kila siku ni mara ya mwisho. Mimi nimemove on na maisha yangu," Lilian alisema.

Derick alijaribu kuomba msamaha na kumhakikishia mwanadada huyo kuhusu upendo wake kwake ila maombi yake hayakusikika.

"Haja gani uishi na mtu hapendi watoto wako. Wakati sina kazi sitakula, wakati niko na kazi ndo nitakula. Yeye akipata zake anaenda kula na wanawake wengine. Nilikuwa nashughulikia kila kitu," Lilian alisema.

Derrick alijitetea akisema, "Kitu ilifanya nipunguze. Si kupenda kwangu nichukue mwenye ako na watoto wawili. Aliniambia mimi kazi yangu ni kulea watoto wa wenyewe, hadi akanitajia majina za baba watoto wake. Alafu pesa ikapunguka."

Lilian alisisitiza kwamba hayuko tayari kurudiana na jamaa huyo na kumtaka aendelee na maisha yake.

"Siko tayari kurudiana naye. Yeye aendelee na maisha yake. Na mimi niendelee na yangu. Yeye ni mtu mkubwa anabehave kama mtoto mdogo. Sitaki maisha yake," alisema.

Kuhusu sababu zake kuchukua vitu vya nyumba, alisema, "Nilijilipa zenye nilikuwa namlisha. Niliuza nikiwa huko kabla niende Mombasa. Aende tu kwa polisi wanitafute, nitajibu tu mbele. Niko Mombasa, Mwembe Tayari, wanitafute hapo nitajibu yote... Na alipe landlord pesa aache kudanganya landlord nilienda na pesa. Siwezi lipa nyumba yenye siishi."

Derrick hakuwa na budi ila kukubali uamuzi wa mwanadada huyo.

Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?