Patanisho: Jamaa aachwa baada ya kuposti mke wa wenyewe kwenye Facebook

Otieno alidai kwamba mwanadada huyo ndiue aliyemposti kwanza akisema anavyomkosa.

Muhtasari

•Otieno alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na mwanadada ambaye alikuwa amepost, alisisitiza kuwa alikuwa akisoma naye.

•Cynthia alipopigiwa simu, alikata mara moja baada ya kuskia anatafutwa na Otieno.

Gidi na Ghost Studioni
Image: RADIO JAMBO

Jamaa ambaye alijitambulisha kama Elijah Otieno ,24, kutoka kaunti ya Siaya alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Cynthia Tamara ,24, ambaye alikosana naye mwezi uliopita.

Otieno alisema uhusiano wake wa miaka mitano uliharibika baada ya mpenzi wake kupata picha ya mwanadada mwingine ambayo aliposti kwenye mtandao wa Facebook.

"Huyo mpenzi wangu tulikuwa tukikaa na yeye. Kuna msichana tulikuwa tunasoma na yeye nilimpost kwenye Facebook. Nilikuwa namtambua tu. Alinitumia picha yake nikamposti. Sikuandika chochote, niliposti tu," Otieno alisema.

Aliongeza, "Vile Cynthia aliona akaniuliza nikamwambia alikuwa classmate yangu. Akakasirika akaenda. Nikimpigia huwa anasema atarudi lakini hajawahi kurudi. Nilikuwa nataka tu nijue vile anaweza kufanya."

Cynthia alipopigiwa simu, alikata mara moja baada ya kuskia anatafutwa na Otieno.

Otieno alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na mwanadada ambaye alikuwa amepost, alisisitiza kuwa alikuwa akisoma naye.

"Huyo ako kwake. Ameolewa. Tulikuwa shule moja, niliona tu nimpost nimtambue. Alikuwa amenipost, pia mimi nikampost. Yeye aliandika 'I miss you my former classmate'," Otieno alisema.

Otieno alishauriwa kusubiri mpenziwe atulie kwanza ili aone kama wataweza kuelewana.

Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?