Patanisho: Jamaa alalamika mkewe kupigiwa simu, kuchat kitandani saa sita usiku

"Tukienda kitandani, anafinya simu saa sita usiku. Nikimwambia afanye kitu anasema hakuja kufanya kazi alikuja kukaa," Evans alilalamika.

Muhtasari

•Evans alisema mahusiano yake ya takriban miezi sita yalisambaratika siku mbili zilizopita kufuatia suala la kutoaminiana.

"Vile alifika kwao, ananipigia simu kudai pesa. Anasema kama siwezi kumtumia pesa nisimpigie simu," Evans alisema.

Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Evans Mweresa ,27, kutoka Nyamira alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Olpah Muturi ,28, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Evans alisema mahusiano yake ya takriban miezi sita yalisambaratika siku mbili zilizopita kufuatia suala la kutoaminiana.

Alidai kwamba mpenziwe amekuwa akizungumza na wanaume wengine mida ya usiku pamoja na kumkosea heshima kwa nyumba.

"Nilikuwa nampata na simu saa tano usiku. Nikimuuliza anazungumza na nani ananipigia kelele. Tukienda kwa kitanda, anafinya simu saa sita usiku. Nikimwambia afanye kitu anasema hakuja kufanya kazi alikuja kukaa," Evans alilalamika.

Aliendelea, 'Nilimwambia sitaki kumpiga aende kwao. Vile alifika kwao, ananipigia simu kudai pesa. Anasema kama siwezi kumtumia pesa nisimpigie simu. Nilimuoa akiwa na mtoto mmoja. Tulikuwa tunapanga tuende nyumbani kuchukua mtoto wake aje tukae. Sasa hivi akipiga simu nikose kushika, anatumia ya mamangu. Ananipigia simu anasema anataka kuenda kwetu. Hiyo ndo kitu inanisumbua."

Evans alisisitiza kujua msimamo wa mpenzi huyo wake na kudai kwamba hana nia ya kurudiana naye kwa sasa.

Hata hivyo, juhudi za kuwapatanisha wawili hivyo ziligonga mwamba kwani Bi Olpah hakushika simu zetu.

Evans alimalizia kwa kumwambia, "Kama umeenda ni sawa. Mimi nilikupenda na mtoto lakini ukaanza madharau."

Gidi alimshauri kutafuta mwanamke mwingine wa kuoa kwani mahusiano yake na Bi Olpah yalionekana kutofua dafu.