logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa amfukuza mkewe mbele ya watoto, majirani baada ya kumcheat mara kadhaa

Gideon alijaribu kumshawishi mkewe ayeyushe moyo yake ili waweze kuendeleza familia ila juhudi zake hazikjufanikiwa.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi22 July 2024 - 06:27

Muhtasari


  • •Gideon alisema ndoa yake ya miaka 8 ilivunjika Januari mwaka huu kutokana na ukosefu wa uaminifu kwenye ndoa.
  • •Gideon alijaribu kumshawishi mkewe ayeyushe moyo yake ili waweze kuendeleza familia ila juhudi zake hazikjufanikiwa.

Gideon Simiyu Shikuku ,27, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na ke wake Catherine Machuma ,26, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Gideon alisema ndoa yake ya miaka 8 ilivunjika Januari mwaka huu kutokana na ukosefu wa uaminifu kwenye ndoa.

Alisema alimfukuza mke wake baada ya kujihusisha na mambo ya mpango wa kando.

"Tulikosana naye Januari kwa mambo ya mpango wa kando. Sio mara yake ya kwanza kukosana naye kwa sababu ya mambo ya mpango. Tangu nimuoe, tumekuwa na matatizo mara kama mbili, tatu. Nilimwambia aende kwao ili hasira zetu zipungue," Gideon alisimulia.

Aliongeza, "Baada ya siku tatu nilipata barua kutoka kwa chifu eti kuna mkutano inafaa iwepo. Yeye hakuwa kwenye mkutano, nilipata babake tukazungumza. Mkutano ilikuwa kuhusu mambo ya kushughulikia watoto. Tuliongea mambo ikaisha. Nilimpigia simu jana,yeye  kuskia sauti yangu akakata simu. Babake aliniambia msichana alienda kazi ya nyumbani Nairobi. Ningependa turudiane ili tuendelee kulea watoto."

Catherine alipopigiwa simu, aliweka wazi kwamba hana nia ya kurudiana na mzazi huyo mwenzake na kumtaka asonge mbele na maisha yake.

"Nilimkataza mimi sitaki mambo yake. Nilimwambia amove on, mimi pia niko na maisha yangu. Mimi nilikataa katakata, hakuna kurudi nyuma tena. Ashughulikie watoto, hiyo nitakuwa sawa. Mimi na yeye iliisha hivyo," Catherine alisema.

Aliongeza, "Nimefungua redio nikasikia jina langu. Nimeshanga sana. Siwezi nikasema nilikuwa na makosa ama yeye alikuwa na makosa. Mimi nikiamua nimeamua. Mtu anakufukuza mbele ya watoto, mbele ya watu wamesimama. Mimi pia niko na machungu yangu. Ukiona tumetoka kwenda kutafuta kazi, lazima kuna kitu imetufinya."

Gideon alijaribu kumshawishi mkewe ayeyushe moyo yake ili waweze kuendeleza familia ila juhudi zake hazikjufanikiwa.

"Mimi nakuomba kama mke wangu, rudisha roho yako nyuma tuendelee na maisha. Upande wangu, nakuchukua kama mke wangu," Gideon alisema.

Mama huyo wa watoto wake wawili alijibu, "Imeisha hivyo.Najua watoto wako, wako wazima. Pia mimi na baba yao tuko wazima. Wacha yeye amove on, na mimi nimove on na maisha yangu. Siwezi kubadilisha..Akikuja kama anataka kuona watoto, anaweza kuja nyumbani awaone. Kurudiana asahau."

Je, maoni yako ama ushauri wako kwa wawili hao ni upi?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved