Jamaa aliyejitambulisha kama Geoffrey Simiyu ,35, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Teresa Wafula ,27, ambaye aliksaoana naye mapema mwaka huu.
Simiyu alisema ndoa yake ya miaka miwili iliharibika Januari 2024 kutokana na mizozo ya kinyumbani ambapo mkewe aliroka pamoja na mtoto wao mmoja.
"Tulikosana kwa sababu ya mashida za nyumbani, tulikuwa tunakosana kidogo kidogo tu. Alikuwa anaenda kukaa kwa majirani tukikosana. Nilipomwambia, akakasirika akaenda nyumbani. Nilijaribu kuenda kwao tutengeneze maneno, haikuwezekana akaenda Nairobi. Anasema tu atarudi lakini hawezi kuniambia wakati atarudi," Geoffrey alisema.
Teresa alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba anapanga kurudi nyumbani baada ya kumaliza mambo ambayo alikuwa akishughulikia.
"Mimi sitaongea kwa redio. Ni heshima tu nimekupea. Mwambie nitakuja," alisema.
Jambo hilo lilionekana kumfurahisha sana Simiyu ambaye alisema, "Nakupenda sana. Naomba urudi nyumbani... Yeye ni moyo wangu, Nikiwa na yeye, naskia niko sawa,"
Teresa alisema, "Mimi pia nampenda. Nampenda kama njugu karanga. Nitakuja nyumbani. Usiwe na wasiwasi, nitarudi nyumbani. Bado nakuhitaji kama mume wangu."
"Mimi mwenyewe niko na sababu. Ungoje mwisho wa mwezi, kama sitakuja ndo unipeleke Radio Jambo," alimwambia.