logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanadada aliyeolewa akiwa na mtoto azaa mwingine nje ya ndoa ya miaka 17, mumewe amsamehe

Geoffrey alisema alimuoa Lilian akiwa na mtoto mmoja, wakapata watatu pamoja, kisha mke wake akazaa mwingine nje.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi25 July 2024 - 06:31

Muhtasari


  • •Geoffrey alisema alimuoa Lilian akiwa na mtoto mmoja, wakapata watatu pamoja, kisha mke wake akazaa mwingine nje.
  • •Aliniambia mimba ni yangu, nilihesabu miezi nikaona haiingiani. Yeye bado anasisitiza mtoto ni wangu," Geoffrey alisema.

Katika kitengo cha Patanisho, mwanaume kwa jina Geoffrey Omar ,37, kutoka Nyamira alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Lilian Nyanduko ,37,  ambaye alitengana naye mapema mwaka huu.

Geoffrey alisema ndoa yake ya miaka 17 ilisambaratika Aprili mwaka huu kutokana na tofauti nyingi za kinyumbani.

Alidai kwamba alikuwa akifungulia mkewe biashara kisha anaiangusha baada ya muda.

"Tumeendelea tu vizuri kutoka nyuma. Ilifika mahali nikaenda kazi nje. Nikafanya kazi na baadaye nikamfungulia biashara, nikimfungulia biashara inafika mahali inaunguka. Ilifika mahali akasema hataki mambo yangu. Sijaenda kwao kwa sababu wakati nilienda nilikuwa karibu kupigwa. Sikupigwa lakini walikuwa karibu kunipiga. Nilienda wakaniitisha mahari, baadaye nililipa," Geoffrey alisema.

Geoffrey alisema alimuoa Lilian akiwa na mtoto mmoja, wakapata watatu pamoja, kisha mke wake akazaa mwingine nje.

"Alipata mtoto mwingine nje, ni mtoto mdogo. Nilikubali na nikamsamehe. Kuna namba nilikuwa napata kwa simu. Sikumuuliza sana kuhusu suala hilo, niliona tutakosana. Mtoto alipata akiwa ndani ya ndoa.

Nilikuwa kazi ya nje kama miezi tatu nje hivi. Nilikaa naye siku tatu hivi, nikarudi kazini, baada ya miezi tatu akaniambia ako na mimba. Aliniambia mimba ni yangu, nilihesabu miezi nikaona haiingiani. Yeye bado anasisitiza mtoto ni wangu," alisema.

Aliongeza,"Alienda na watoto wote. Alafu kufika nyumbani kwao akafukuza hao watatu ambao tulipata naye akawapandisha pikipiki akawaambia waende kwao. Sasa hivi wako nyumbani. Niulitaka kujua msimamo wake kwa sababu nilikuwa nimelipa mahari. Sio eti nilikuwa nataka kurudiana naye sana."

Juhudi za kurejesha ndoa ya Geoffrey hata hivyo hazikufanikiwa kwani mzazi huyo mwezake alikata simu.

"Inaweza kuwa mkora," aliambia Gidi kabla ya kukata simu.

Geoffrey alisema, "Kuna pesa ya chama naskia alichukua akatoroka. Huenda hataki kuongea anafikiria watu wao wanampigia. Akiwa nyumbani alichukua loan akatoroka nayo.Wakati alienda alinitukana vibaya. Nilikuwa nataka kujua msimamo wake."

Katika ujumbe wake wa mwisho kwa Lilian, Geofrey alisema, "Hao watu wa kwao kama wamemwambia maneno anaona yanaweza kumsaidia, ni sawa tu, aendelee kulinda hao watoto alienda nao."

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved