Patanisho: "Hii mambo ya kupanisha Gen Z, inahitaji allowance!" Gidi asema baada ya wapenzi kutoelewana

"Mimi mahali niko, niko salama. Sina stress vile nilikuwa nayo nikiwa kwako.Mimi nishamove on, ata yeye amove on ," Rose alisema.

Muhtasari

•Enock alisema ndoa yake ya chini ya mwaka mmoja ilivurugika wiki jana wakati mkewe baada ya mkewe kuona mazungumzo yake na mfanyikazi mwenzake.

•"Naomba serikali itupatie Gen-z allowance. Hii mambo ya kupanisha Gen Z, inahitaji allowance," alisema Gidi. 

Ghost na Gidi studioni
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Enock Ogaki Nyang'au ,24, kutoka Nyamira alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Rose Kerubo ,22, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Enock alisema ndoa yake ya chini ya mwaka mmoja ilivurugika wiki jana wakati mkewe baada ya mkewe kuona mazungumzo yake na mfanyikazi mwenzake.

"Kuna video ya tiktok tulichukua na rafiki huwa tunafanya naye kazi. Kisha mpenzi wangu aliona chat tukiongea na huyo mfanyikazi mwenzangu akakasirika akaenda. Huyo mwenzangu alikuwa ananiuliza kama nimeenda kazi, nikamwambia sijaenda, akaniambia nikienda nipitie kwake nikimchukua. Kitu ilimkasirisha zaidi, huyo msichana alikuwa anasema nimlipie simu, ako na simu ya lipa mdogo mdogo. Hapo ndo shida ilianza, huyu msichana akaenda," Enock alisema.

Rose alipopigiwa simu mara ya kwanza, alikata mara moja baada ya Gidi kujitambulisha.

Enock aliendelea kueleza huzuni yake baada ya kutemwa na mpenziwe.

"Ata sijaenda kazi, niko na mawazo mbaya," alisema.

Aliongeza, "Nimemuoa rasmi. Mahari bado. Nilimtoa kwa wazazi. Hadi wazazi wanajua. Wazazi wanampigia simu, anakataa kushika. Hata watu wa kwao hawajui mahali ako. Na alitoka usiku. Nikitoka kazi alikuwa anauliza nimefika wapi, kufika kwa nyumba nikapata hayuko."

Rose alipopigiwa simu mara ya pili, alisema, "Mimi mahali niko, niko salama.Mwambie amove on. Madharau alikuwa ananifanyia, akae na huyo msichana alikuwa na yeye. Mimi nishamove on, ata yeye amove on. Alikuwa anasema ameacha, lakini anaendelea. Anasema ameacha alafu naona video kwa tiktok wakiwa kwa hoteli wakila chips."

Enock alijaribu kujitetea akisema, "Nilikosea, namuomba msamaha. Rose mi nakupenda yangu yote. Nakuomba tafadhali urudi."

Rose alisema, "Mimi sitaki msamaha. Alikuwa anaenda hadi kwake. Mimi mahali niko, niko salama. Sina stress vile nilikuwa nayo nikiwa kwako. Kesho naenda nyumbani. Ulikuwa hadi unanichapa alafu unaanza kupigia huyo msichana. Ulikuwa unanichapa alafu unasema hata nikienda huwezi kunitafuta. Kwa nini tena unanitafuta?"

Enock alisisitiza mapenzi yake kwa mpenziwe na kumuomba arudi.

"Atulize akili alafu aniambie uamuzi wake," alisema.

Rose hata hivyo alishikilia msimamo wake wa kutorudi.

Gidi alishangazwa na wawili hao a akasema

"Naomba serikali itupatie Gen-z allowance. Hii mambo ya kupanisha Gen Z, inahitaji allowance," alisema Gidi. 

Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?