"Niliona ni handsome nikapita naye!" Mwanadada atoka kimapenzi na rafiki ya mumewe baada ya kuhamia kwao

"Sasa huyo rafiki yake bado ako kwa nyumba.Kama ashaniletea bwana kwa nyumba, si uache niendelee," Kevin alisema.

Muhtasari

•Kevin alisema ndoa yake ya miaka minane ilianza kusambaratika baada ya mkewe kumpata na msichana mwingine.

•" Yeye analeta wanaume kwa nyumba, akileta mwenye ni handsome, si unapita tu na yeye. Huyo jamaa sasa amekaa tu, anaangalia mpenzi wake, si ashapata bibi," Mary alisema.

Ghost na Gidi studioni
Image: RADIO JAMBO

Kevin Sang ,31, kutoka Dandora alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Mary Mueni ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Kevin alisema ndoa yake ya miaka minane ilianza kusambaratika baada ya mkewe kumpata na msichana mwingine.

Alifichua kwamba baadaye mkewe alianza mahusiano na mmoja wa marafiki zake ambaye alileta kwa nyumba.

"Kuna siku nilikuwa na msichana tunatembea kwa barabara, mke wangu akanipata  nikiwa na yeye.Mwanadada  huyoalikuwa mpenzi wangu. Ndio tulikuwa tunaongea ongea. Bado ilikuwa kujuana  Kufika kwa nyumba baadaye, tukaongea na mke wanbgu. Nikamuomba msamaha akakataa kwanza. Baadaye akanisamehea tukarudiana," Kevin alisimulia.

Kevin aliendelea," Kuna wakati rafiki yangu akatoka ushago, nikamkaribisha kwa nyumba. Mke wangu  akaanza mahusiano na rafiki yangu. Mimi nikatoka nikawaachia nyumba. Kwa sasa mimi niko Kariobangi, mke wangu ako kwa nyumba na huyo jamaa. Mimi nilienda nikawaachia nyumba. Sasa mke wangu ndiye analipa nyumba.Ningetaka kujua kama ameamua kukaa na yeye aniambie. Vitu zangu zingine ziko huko. Nilienda, huyo jamaa akanitishia kuenda kwa polisi. Nikaona badala ya vita, niondoke."

Mary alipopigiwa simu, alibainisha mumewe ndiye aliyechukua virago vyake akaenda baada ya kumleta rafikiye kwa nyumba.

Aidha, alithibitisha kwamba ni kweli aliamua kutoka kimapenzi na rafiki ya mumewe.

"Yeye ndiye alipanga virago zake akaenda. Alianza kuwa na wamama wengine. Alikuwa ananipita tu kwa barabara akiwa amewashika kiuno. Yeye akawa analeta marafiki zake kwa nyumba. Baadaye akakuja akatoroka na vitu zake. Sasa mimi ningefukuza rafiki yake aje? Sasa huyo rafiki yake bado ako kwa nyumba.

Kama ashaniletea bwana kwa nyumba, si uache niendelee. Mimi sio mawe. Yeye anabeba wanaume analeta kwa nyumba. Na sio mmoja ama wawili," Mary alisema.

Aliendelea, "Yeye ako na wasichana kwa barabara. Wewe uko tu kwa nyumba. Yeye analeta wanaume kwa nyumba, akileta mwenye ni handsome, si unapita tu na yeye. Yeye ndiye alineletea, akule hiyo na akule huu. Mimi niliona ni handsome, nikapita na yeye. Yeye hajui majukumu. Huyo jamaa sasa amekaa tu, anaangalia mpenzi wake, si ashapata bibi."

Mary pia alidai kwamba licha ya kuwa kwenye ndoa kwa miaka nane, mumewe hajawahi kupelekea familia yake kwao.

"Mama yake hajawahi kutembea kwetu. Kama hanionyeshi madharau singekuwa hivyo. Yeye amezaa nje. Sasa punda amechoka na ameweka mzigo chini," alisema.

"Nilikuja nikapata mimba mwaka jana, ikawa na shida, ilibidi itolewe. Nilikuwa nampenda m yeye siku zote alikuwa ananicheza na wasichana. Alikuwa analeta wasichana kwa nyumba, navumilia. Alikuja juzi wakaongea, akamwambia rafikiye amempea Mary bure, na mimi nikakubali tu," aliongeza.

Je, una maoni ama ushauri upi kuhusu Patanisho ya leo?