•Kennedy alisema ndoa yake ya miaka miwili ilisambaratika mwaka jana wakati mke wake aliondoka nyumbani kwenda chuo.
•Kennedy hata hivyo alimsihi hewani amwambie ukweli ili ajue hatua bora ya kuchukua.
Kennedy Opwora ,27, kutoka Mumias alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Anjela Ominyo ,24, ambaye alimuacha mwaka jana.
Kennedy alisema ndoa yake ya miaka miwili ilisambaratika mwaka jana wakati mke wake aliondoka nyumbani kwenda chuo.
"Hatukukosana na mke wangu. Nilimchukua 2021 tutkakaa naye nyumbani tukapata mtoto. Tukaelewana anataka kuenda chuo kusoma. Alikuwa anaenda kusoma alafu anakuja kutembea nyumbani. Baada ya mihula miwili alichukua mtoto akasema anataka kupelekea mamake. Nikamuuliza kwa nini akasema chuo chao kiko karibu na nyumbani kwa hivyo ingekuwa rahisi kwake," Kennedy alisimulia.
Aliongeza, "Kwa sasa amekawia huko sana na ata harudi jinsi alivyokuwa akirudi kitambo. Wakati mwingine huwa anasema nimtumie nauli akuje na mtoto. Baada ya kumtumia nauli ananiblock. Mara ya mwisho tuliongea ni mwezi wa sita ambapo aliniambia nisahau mambo ya watoto eti yeye akimaliza shule atalea mtoto peke yake. Alisema penye yake ako stable na ako na uwezo wa kulea mtoto wake hahitaji usaidizi wangu. Sijui kama alifika huko akaona mazuri, simuelewi."
Juhudi za kumpatanisha Kennedy na mpenziwe hata hivyo hazikufua dafu kwani Anjela hakushika simu alipopigiwa na Ghost.
Kennedy hata hivyo alimsihi hewani amwambie ukweli ili ajue hatua bora ya kuchukua.
"Wewe ulikuwa mke wangu na sikuwahi kufukuza. Ulitoka tu ukaenda shule. Kama ulipata mtu mwingine ni sawa, tafuta vile tutalea mtoto pamoja. Kama mtoto amekuwa mzigo mlete nitalea. Na kama mtoto hakuwa wangu kuja uniambie nitaelewa.
Kama huwezi kuolewa na mimi niambie niko tayari kuambia Radio Jambo initafutie mwanadada anataka kuolewa niolewa. Aliambia mama na dada zangu kwamba ni yeye atataka kuleta mtoto," alisema.
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?