Katika kitengo cha Patanisho, Elvis Situma, mwenye umri wa miaka 23 alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na nyanya yake Neddy Nekesa ambaye alimlea.
Situma alisema uhusiano wake na nyanyake uliharibika kufuatia mzozo kuhusu pesa ambapo alijipata amemuongelesha vibaya.
"Ilikuwa ni mambo kuhusu pesa. Shosho yangu alinilea tangu nikiwa mtoto. Mama ako lakini nimezoea kuishi na nyanya. Karo yote ya shule alikuwa analipa. Nimemaliza shule nikaja kutafuta Nairobi. Pesa ikawa ngumu kidogo kupata na nyanya kuna pesa alikuwa anahitaji haraka, mimi sikuwa tayari na hiyo pesa. Akaniuliza mbona simtumiangi pesa na wazazi waliniacha yeye ndiye amenilea. Nikamwambia sijakataa. Nikashtukia nimemwambia wewe kashere acha mchezo wako sasa hivi sina nikipata nitakutumia. Mpaka wa leo hajawahi kunipigia simu. Huwa napiga simu hashiki. Nilikuwa natamani tu tuwe na mazungumzo mazuri ili hii Disemba nimtembelee," Situma alisema.
Nyanyake Situma alipopigiwa simu, mwanzoni alikataa kuzungumza naye kabisa.
Kwa uchungu, alifunguka jinsi mjukuu wake alimuongelesha vibaya baada ya kumuomba pesa za dawa.
"Hii ni maajabu ya Musa. Huyo mtoto ni mimi nililea. Mamake alimzaa angali shule, na akaoelewa kwingine. Nikasema siwezi tupa mtoto. Nilijinyima kila kitu nikasomesha huyo mtoto. Nikaona nisaidie mtoto labda huko mbele atasaidia mamake. Mtoto akasoma vizuri akaenda kazi," Bi Nekesa alisema.
Aliongeza, "Mimi shida niko nayo, niko na magonjwa mingi kwa mwili yangu. Hii kitu ni gharama. Wajomba wake wameshindwa kuununua dawa. Nikapigia mtoto simu aninunulie dawa, hataki kushika. Akishika, ananiongelesha kwa madharau. (Akianza kulia). Mungu asamehe huyu mtoto. Nilimpigia simu akaniambia "ongea haraka niko kazi". Mtoto ambaye nimesomesha shule mpaka nikauza ng'ombe ili asome. Nilikuwa nimesema huyu mtoto nimemtoa kwa akili yangu. Mimi sikuwa namuomba pesa ya kutumia, nilikuwa namuomba ya dawa tu. Lakini mtoto alikuwa ananiongelesha kwa madharau."
Situma alipoanza kuomba msamaha, nyanyake alimwambia ,"Wewe usiniite shosho. Niite jina, mimi sio nyanya yako. Ulifika wapi mpaka ukajua umekosea?"
"Huku Nairobi kupata pesa sio rahisi. Nilikuwa nang'ang'ana nipate pesa ili nikutumie, Lakini nikapatwa na shjda fulani ikabidi nitumie. Nilikuwa tu na hasira na nilikuwa kazini," Elvis alimjibu.
Nyanyake alimwambia, "Mbona hukunieleza baadaye? Ulijua mtu ulikuwa unajibu? Unajua baraka ama laana utatoa kwangu. Lakini shukuru Mungu mimi ni Mkristo. Singekubali msamaha wako."
Bi Nekesa hata hivyo alikubali kuyeyusha moyo wake na kumualika nyumbani.
"Kama kweli umejuta, nakukubali nyumbani uje uombe msamaha nyumbani sio kwa redio.. Nitamsamehe, nilikuwa nimemfuta kutoka kwa roho yangu," alisema.
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?