(Video) Jamaa aachwa kwa kunywa pesa za mkewe na na kumtishia kwa panga na nyundo

Muhtasari

•Wanjala alisema ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika mwezi Januari baada yake kurudi nyumbani akiwa mlevi chakari na kuibua mzozo na mkewe.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Christopher Wanjala (26) alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mkewe Nancy (26) ambaye walitengana naye kufuatia mzozo wa kinyumbani.

Wanjala alisema ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika mwezi Januari baada yake kurudi nyumbani akiwa mlevi chakari na kuibua mzozo na mkewe.

Nancy alichukua watoto wao wawili na kurudi kwao nyumbani baada ya kugura ndoa yake na Christopher.

Tazama jinsi Patanisho ilivyokuwa:-