Patanisho: "Alichukua silaha akanidunga kichwani" Mwanapolisi afunguka maovu ya mkewe

Humphrey alidokeza kuwa Stella alitenda makosa mengi wakati wa ndoa yao ya nusu mwongo.

Muhtasari

•Stella alisema alitengana na mumewe baada ya kutoka nje ya ndoa na kujihusisha kimapenzi na rafiki yake wa muda mrefu.

•Humphrey hata hivyo alibainisha kuwa tayari amesonga mbele na maisha yake na hataki uhusiano na Stella.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Bi Stella Otieno ,24, kutoka Zimmerman alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Humphrey Otieno ,25, ambaye alikosana naye mwaka jana.

Stella alisema alitengana na mumewe ambaye ni afisa wa polisi baada ya kutoka nje ya ndoa na kujihusisha kimapenzi na rafiki yake wa muda mrefu.

"Tulikuwa tunavurugana alafu tukatengana. Nilimcheat na rafiki wa muda mrefu. Siku moja alikuja kwa nyumba nikiwa kazini alafu akanitumia picha za mzigo nilikuwa nimetumiwa  alizopata kwa simu. Alifanya uchunguzi wake, baadaye wakafanya conference call tukaongea na wote," alisimulia.

Stella alisema mumewe alianza kumfuatilia baada ya kushuku kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.

"Baada ya muda, alianza kuja kunivamia kazini. Alianza kunitafuta, alikuwa anitafuta hanipati. Wakati mmoja alienda kwa dadangu akapata siko, Aliniambia nihame mahali nilikuwa. Kuna siku alinipigia akiniambia vile nilimkosea,"

Alifichua kwamba alikuwa amekaa kwenye ndoa na Bw Humphrey kwa miaka mitano na tayari walikuwa na mtoto mmoja pamoja.

Humphrey alipopigiwa simu, mzazi huyo mwenzake alichukua fursa kuomba msamaha kwa makosa yote aliyotenda.

"Niko kwenye magoti yangu.Tafadhali kubali msamaha wangu turudiane. Naomba msamaha kwa vitu zote ambazo nilifanya," alisema.

Humphrey alifichua kuwa tayari alikuwa amemsamehe mke huyo wake wa zamani mara nyingi na kubainisha hana kinyongo naye.

"Sina shida na wewe. Mimi nashindwa unataka niseme nini. Hii msamaha nimekusamehe mara nyingi," alisema.

Humphrey alidokeza kwamba mzazi huyo mwenzake alitenda makosa mengi wakati wa ndoa yao ya nusu mwongo.

Alibainisha kuwa hakufurahishwa na jinsi wanafamilia wa mkewe waliegemea upande wake kila alipojaribu kusuluhisha mzozo wao.

"Hii msamaha ameomba sana. Ata nimeenda kwa watu wao sana. Wakati kitu imefanyika, watu wa kwao hawawezi kusikiliza," alisema.

Alidokeza kuwa mkewe alikuwa anachochewa na dada yake kuwa na uhusiano na rafiki huyo wake wa muda mrefu.

Pia alifichua kwamba Stella aliwahi kumvamia na kumjeruhi kichwani wakati walipokuwa wakizozana.

"Kitu kubwa, hakuwa na heshima kwangu. Hakukaa na mimi kama mume wake. Aliharibu vitu sana kwa nyumba.  Wakati moja alichukua silaha akanidunga nayo kwa kichwa. Niliambia wanafamilia wake lakini hakuna mwenye alisimama na mimi. Nimevumilia sana na yeye. Hata kuna watu walikuwa wanasema niachane na yeye. Mimi nilivumilia tu. Yeye mwenyewe anajua," alisema Humphrey.

Huku akijitetea, Stella aliweka wazi kuwa tayari amerekebisha makosa ambayo alitenda dhidi ya mume wake.

Humphrey hata hivyo alibainisha kuwa tayari amesonga mbele na maisha yake na hataki uhusiano na Stella.

"Sina bibi lakini sitaki mambo ya mapenzi na huyo msichana," alisema.

Je, una ushauri gani kwa wawili hao?