Patanisho: Mke abeba sufuria, nguo baada ya kumfumania mumewe na Ex wake

Muhtasari

•Kibet alisema baada ya mkewe kumfumania aligura ndoa yao ya miaka mitano na kubeba watoto wao wawili baada ya kumtupia cheche za maneno.

•Kibet pia alisema mkewe alimshtumu kwa kudanganya majina baada ya kugundua jina lake la utani.

Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost Asubuhi, jamaa aliyejitambulisha kama Leonard Kibet ,28, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mkewe Winnie Jeruto ,22, ambaye alimuacha baada ya kumfumania na mpango wa kando.

Kibet alisema baada ya mkewe kumfumania aligura ndoa yao ya miaka mitano na kubeba watoto wao wawili baada ya kumtupia cheche za maneno.

"Nilipatikana kona mbaya. Huyo mrembo ambaye alinipata naye alikuwa ex wangu. Alikuwa ananijulia hali tu kwa kuwa hatukuwa tumepatana miaka mitano. Tulikuwa tunaongea naye mke wangu akatupata tukiongea alipokuwa anatoka mtoni. Alikasirika akabeba kila kitu mpaka sufuria alizokuwa amenunua, nguo zake na vitu zingine," Kibet alisema.

Kibet pia alisema mkewe alimshtumu kwa kudanganya majina baada ya kugundua jina lake la utani.

"Mimi nilikuwa mchezaji kandanda. Nilikuwa na majina mengi, watu walikuwa wananiita Wembe. Aliposikia hilo jina alidhani mimi ni mtu mbaya. Nilikuwa nawajibika kila kitu. Alikuwa anapata kila kitu," Kibet alisema.

Winnie alipopigiwa simu alisema alikasirika sana baada ya kumpata mumewe barabarani na mpenzi wake wa zamani.

"Mi nilikasirika nikachukua vitu zangu nikaenda nyumbani. Ata simu yake iko na password na huwa haweki chini, sasa sijui kama huwa wanaongea. Wakati niliwapata nilidhani huwa wanaongea. Mi nilikasirika nikaona nichukue vitu nimenunua nimuachie hizo zingine huenda akapata huyo ex wake," Alisema Winnie.

Kibet alijitetea kwa kusema yeye na mpenzi wake wa zamani walikuwa wanajuliana hali tu na hakuwa na mpango wowote mbaya naye.

"Sikuwa na nia mbaya. Nilikuwa namsalimia tu kama mtu najua . Hatukuwa na mpango mbaya" Alisema.

Winnie alikubali kumsamehe mumewe na kurudiana naye kwa masharti kuwa hatarudia makosa yake.

Kutokana na hayo Kibet alikubali kula kiapo huku akiahidi kuwa mwaminifu kwa mkewe na kutozungumza na Ex wake.

"Mi nakupenda kama baba ya watoto wangu. Na usinifanyie hivo tena. Mi nakupenda kama Water Melon," Winnie alimalizia kwa kusema.