Nilienda kwa mganga kufilisisha biashara ya mtu lakini akakua wazimu-Mwanamume asimulia haya

Muhtasari
  • Mwanamume afichua jinsi alienda kwa mganga na uganga wake kuleta maafa makubwa
Teke Teke:Mbusi na Lion
Image: Studio

Katika kipindi cha toboa siri cha mtangazaji Mbusi na Lion, mwanamume mmoja alipiga simu na kutoboa siri jinsi alivyo mfanya bwana wa wenyewe wazimu badala ya kufilisisha biashara yake.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilikuwa na jrani yangu ambaye alikuwa anafanya biashara, ilikuwa inaendelea vyema nilihisi vibaya na kujawa na wivu

Iliniweze kufilisisha biashara yake nilienda kwa mganga, aliniambia anataka mahindi kilo tano, na elfu tano nilimpa vitu hivyo

Baada ya hayo alinipa mbengu kama za ndegu na kuniambia niende nikaeke mahali mzee huyo alipokuwa anafanyaia biashara yake

Badala ya biashara yake kufilisika, alikuwa wazimu, saa hizi yuko nyumbani na familia yake imeishiwa na pesa kwa maana wamekuwa wakimpeleka hospitali tofauti." Alieleza Mwanamume huyo.

Mwanamume huyo alisema kwamba anataka kutoboa siri hiyo kwa maana alihisi vibaya baada ya mzee huyo kuwa wazimu.

Pia alifichua alipoenda kumuuliza mganga huyo nini haswa kilienda mrama alisema kwamba alitumia dawa hiyo kupita kiasi huku akimwambia hamna kitu anaweza kufanya kwa sasa.